Ikiwa leo ni kilele cha
siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa malaria duniani wananchi mkoani Geita
wametakiwa kuacha tabia ya kutumia dawa
kabla ya kupata vipimo pindi wanapohisi kuugua na badala yake kufika katika vituo vya afya ili waweze
kupatiwa tiba sahihi.
Hayo yamebainishwa leo
na mratibu wa udhibiti wa malaria mkoani Geita bi Veronica Mazigi alipokuwa
akizungumza na Storm habari baada ya kutembelea ofisi za Storm fm zilizopo
mkoani hapa.
Ameongeza kuwa wananchi
wanapaswa kuachana na dhana potofu ya kudai kuwa vyandarua vinavyotolewa na na
mashirika pamoja na wadau mbalimbali vimekuwa vikisababisha upotevu wa nguvu za
kiume jambo ambalo halina ukweli wowote.
Aidha bi Mazigi amesema
wananchi wanatakiwa kubadilika kwa kuwa
na muitikio chanya kwani ugonjwa huo ni tatizo kubwa kuliko tatizo lingine
kitaifa kwa kufuata utaratibu wanaopewa
ikiwa ni pamoja na kulala katika
vyandarua hali ambayo itasaidia kupunguza vifo
vitokanavyo na malaria nchini.
Katika hatua nyingine maadhimisho ya
mwaka huu, wizara ya afya imepanga kuendelea
kutoa elimu kwa jamii juu ya njia mbalimbali za kijikinga na malaria pamoja na maradhi mengine
ya kuambukiza yatakayowajumuisha viongozi wa wizara ya afya, wa mikoa , wilaya
na vikundi mbalimbali vya mazoezi pamoja na viongozi wa taasisi za chama na
serikali huku kauli mbiu ya maadhimisho
hayo ikisema ‘maliza malaria kabisa’.
No comments:
Post a Comment