Mvua na nguzo za Tanesco
kuwa ndani ya barabara ya jimboni mkoani Geita
ni sababu ambazo zimepelekea kuchelewa kukamilika kwa wakati ujenzi wa
barabara hiyo yenye kilomita 2.2.
Mkuu wa mkoa wa geita meja
jenereali mstaafu Ezekiel Kyunga ameeleza sababu hizo ofisini kwake wakati akizungumza na Storm habari kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mbunge wa
jimbo la Geita vijijini mh Joseph Msukuma hivi karibuni katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato mbele ya Rais wa
Tanzania dk. John Pombe Magufuli, ambapo mbunge huyo alidai kuwa
mkandarasi wa kampuni ya Jasco ya jijini
Mwanza anayejenga barabara hiyo ameshindwa kukamilisha kwa wakati.
Mh kyunga, amesema zipo
sababu za msingi zilizochelewesha barabara hiyo ambapo baadhi ya mambo yaliyokwamisha
kutokamlika kwa ujenzi wa barabara hiyo ni pamoja na mvua ambazo zinaendelea
kuyesha mkoani Geita.
Katika hatua nyingine mh
Kyunga amesema kuwa katika kikao cha RCC kilicho keti mwezi disemba mwaka jana chini ya mkuu wa
mkoa aliyekuwepo bi. Fatuma Mwassa waliingiwa na wasiwasi juu utekelezaji wa
mradi huo.
Aidha kwa upande wao
wananchi wamepongeza kwa ujenzi wa barabara hiyo kuwa kiwango kinachotumika kwa
kujenga ni cha uhakika huku wakimwomba mkandarasi huyo kupanua zaidi.
Barabara hiyo inayofadhiliwa na benki ya dunia, ujenzi
wake ulianza mwezi julai mwaka jana na unatarajia
kukamilika mwezi huu licha ya chanagmoto zilizopo katika kukamilisha mradi
huo, huku barabara hiyo ikisubiriwa kwa
hamu na wananchi kwani itaondoa kero
na adha zilizopo.
No comments:
Post a Comment