Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuwauwa Majambazi watatu katika Majibizano ya Risasi,huku moja likifanikiwa kutoroka kwa kutumia Pikipiki ambayo haikuwa na usajili.
Tukio hilo limetokea jana April 12 majira ya saa 12 jioni katika
Mtaa wa Msikiti mkuu ,barabara ya Tabora mjini Kahama ambapo Majambazi hao
wakiwa na silaha za moto.
Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani shinyanga iliyotolewa na
kusainiwa na kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Dismas Kisusi kwa niaba
ya kamanda wa Polisi mkoani humo Mika Nyange imeeleza kuwa mfanyabiashara
aliyefahamika kwa jina la Emmanuel mkumbo mfanyabiashara wa bidhaa za jumla
mjini Kahama alivamiwa na kupigwa risasi kifuani na kichwani baada ya kukaidi
agizo aliloamrishwa na majambazi hao la kuwapatia fedha
Mbali na mfanyabiashara huyo kuuawa mpita njia aliyefahamika kwa
jina la Seleman Shaban alipigwa risasi na majambazi hayo yakiwa katika
majibizano ya Risasi na Jeshi la Polisi ambapo alipata majeraha na kukimbizwa
katika Hospitali ya wilaya ya Kahama ambapo amefariki akiwa anapatiwa matibabu.
Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha
mbalimbali za kivita zilizokuwa zikitumiwa na Majambazi ambazo ni pamoja na
Bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili 1996-AFU 2297,bunduki aina ya UZIGUN
yenye namba za usajili 3452, Magazini 3 za SMG, Risasi 30 zinazotumika katika
bunduki ya SMG na Risasi zingine 30 za UZIGUN, Mabomu mawili ya kurushwa kwa
mkono na Kisu kimoja cha kijeshi.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni Pikipiki mbili, moja aina ya
SanLG namba zake za usajili ni T959 CAE yenye Chesis namba LBRSPJ51C900191,na
nyingine ambayo haikuwa na namba za usajili ikiwa imefutwa namba za
Chesis
Katika uvamizi huo Majambazi hawakufanikiwa kuchukua kitu chochote na Jeshi linaendelea kumtafuta Jambazi mmoja wa Kike ambaye alifanikiwa kukimbia katika tukio hilo,huku maiti za Majambazi hao zikiwa zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maitiHospitali ya wilaya ya Kahama.
KWA PICHA ZA MAJAMBAZI WALIOUAWA
TAZAMA HAPA CHINI.
VIONGOZI
MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mkuu wa Upelelezi wilayani Kahama George Bagyemu akionesha
moja ya Risasi inayotumika katika Bunduki ya UZIGUN iliyokuwa ikitumiwa na
Majmbazi
|
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama
ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Vita Kawawa akizungumza na waandishi wa
Habari wakati akilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kuyauwa majambazi
hayo na kukamata silaha zilizokuwa zikitumiwa na majambazi hayo
|
Mkuu wa Upelelezi wilayani Kahama George Bagyemu akionesha
moja ya bomu la kurushwa kwa mkono lililokamatwa na Jeshi hilo kabla
halijatumiwa na majambazi
|
Mbunge wa jimbo la Kahama Jumanne Kishimba wakati akizungumza
kulipongeza Jeshi la Polisi kwa mapambano dhidi ya uhalifu wilayani Kahama.
|
SILAHA
ZILIZOKAMATWA
No comments:
Post a Comment