Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu mkoani Geita
wameiomba serikali kujenga choo
katika soko hilo ili kuondoa kero
ikiwemo harufu mbaya inayotokana na watu
kujisaidia katika mifuko na makopo ya maji jambo ambalo linahatarisha afya zao.
Wakizungumza na Storm habari wafanyabiashara hao
wamesema serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka juu ya jambo hilo kwani
wanalazimika kufanya hivyo kutokana na kukosa choo katika soko hilo na baadae
humwanga uchafu huo katika mitaro iliyopo sokoni hapo pindi mvua zinaponyeha.
Katibu wa soko hilo bw, Adriani Rwechungula amekiri
kuwepo kwa changamoto hiyo, huku akidai kuwa jambo hilo linatokana na baadhi ya
watu kutokuwa na uelewa juu ya utunzaji wa mazingira ambapo amesema
wafanyabiashara wote sokoni hapo wanatakiwa kushirikiana kuweka mazingira safi
ili hata wanunuzi wa bidhaa wanapoingia sokoni humo wafurahie huduma zao.
Aidha Storm habari imezungumza na afisa afya wa
halmashauri ya mji wa Geita bw, Mabela Ezekiel Mabela ambapo amesema kuwa
serikali inafanya utaratibu wa kutatua
jambo hilo huku akiwataka wananchi kutumia choo cha kulipia kilichopo karibu
na maeneo ya soko hilo wakati serkali iktafuta ufumbuzi wa suala
hilo.
Aidha Mabela ametoa wito wa wafanyabiashara wa soko
hilo kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba yeyote atakaebainika kufanya kitendo
hicho serikali haitosita kuchukua hatua kali za kisheria juu yake ikiwepo
kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment