Wazazi mkoani Geita
wametakiwa kujenga desturi ya kuhakikisha kuwa wanawapeleka kwenye chanjo
watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ili kudhibiti magonjwa ya milipuko ambayo
yamekuwa yakiwakabili watoto.
Akizungumza katika
uzinduzi wa chanjo ya watoto uliofanyikia katika hosptali ya upendo iliyopo
kata ya bomba mbili, mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole Charles Fikiri,amesema
kuwa chanjo ni muhimu sana kwa watoto ambao wapo chini ya umri wa miaka mitano.
Hata hivyo muuguzi
mfawidhi wa zahanati ya Upendo Lyidia
Bwanakunu ameeleza kuwa wamekuwa
na wakati mgumu kutokana na kutoa huduma
bure kwa akina mama wajawazito na watoto
hali ambayo imekuwa ikisababisha mlundikano
mkubwa hivyo ameiomba serikali
kuhakikisha kuwa inatoa ushirikiano
ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa .
Kwa upande wake Anastazia
Shabani ambae ni moja katika ya wazazi waliofika katika huduma ya chanjo
amesema kuwa ni vyema kwa wazazi wengine kuachana na imani ambazo ni
potofu hivyo ni muhimu kuwaleta
watoto kupatiwa chanjo.
Mkurugenzi wa
zahanati hiyo Deogratias Katunzi
ameiomba serikali kutoa msaada wa wauguzi kutokana na kwamba wao wamekuwa
wakijitolea kwa kutoa huduma ya afya kwa watoto na akina mama bure kwa kata mbili.
No comments:
Post a Comment