Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amewataka makatibu tawala wa mikoa nchini kuchukua hatua kali dhidi ya
wote waliosababisha kuwapo kwa watumishi hewa.
Amesema suala hilo la
watumishi hewa limeisababishia Serikali hasara kubwa, hivyo ni lazima watu wote
waliohusika katika sakata hilo wabainishwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa
sheria.
Majaliwa alisema hayo
jana alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi iliyowasilishwa
na mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya pili
kikazi wilayani Ruangwa.
Wakati akiwaapisha
wakuu wapya wa mikoa Machi 15, Rais John Magufuli aliwapa siku 15 kuhakikisha
wanabaini watumishi hewa wote katika mikoa yao na kuwaondoa katika mfumo wa
malipo.
Baada ya kufanyika kwa
kazi hiyo, jumla ya watumishi hewa 7,795 walibainika ambao wameisababishia
Serikali hasara ya Sh7.5 bilioni.
Awali, Zambi alisema
Lindi ina jumla ya wafanyakazi watoro 57 na hewa saba ambao walifariki na
wengine kustaafu, lakini walikuwa wakilipwa mishahara na kuisababishia Serikali
hasara ya Sh36 milioni kwa mwezi.
No comments:
Post a Comment