Siku moja baada ya
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema
ukweli, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Hawa Ng’humbi ameiruka taarifa ya kutokuwapo
kwa watumishi hewa, ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.
Mkoa wa Shinyanga
unaundwa na wilaya tatu ambazo ni Shinyanga, Kishapu na Kahama zinazoundwa na
halmashauri sita ambazo ni Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Mji wa Kahama,
Ushetu, Msalala na Shinyanga Vijijini.
Rais John Magufuli
juzi alitengua uteuzi wa Kilango, ikiwa ni siku 30 tangu alipotangaza kumteua
kwa maelezo kuwa alitoa taarifa isiyo ya kweli kuwa Shinyanga hakuna watumishi
hewa kabla ya kujiridhisha.
Pamoja na
Kilango, Rais Magufuli pia alitengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Shinyanga,
Abdul Dachi, kwa sababu hiyo ya kutoa taarifa za uongo.
Dk Magufuli
alichukua uamuzi huo baada ya kutuma timu mkoani Shinyanga kufanya uhakiki na
kubaini kuwa kulikuwa na watumishi hewa 45 katika wilaya moja ya Shinyanga
kabla ya kwenda wilaya nyingine za Kahama na Kishapu.
Akizungumzia sakata
hilo jana baada ya uamuzi wa Dk Magufuli, Ng’humbi alisema taarifa za
kukosekana watumishi hewa kwenye wilaya yake alizisikia kwenye taarifa ya
habari ya televisheni Machi 30 na zilimshtua.
“Binafsi nilishtuka sana nilipoona
ikitangazwa kuwa mkoa mzima wa Shinyanga, hakuna mfanyakazi hewa wakati mimi
sikuwa hata nimeona taarifa kutoka wilayani kwangu iliyoandaliwa na uongozi wa
halmashauri,” alisema
Ng’humbi.
“Nilijiuliza taarifa imefikaje kwa mkuu wa mkoa bila kupitia kwangu?
Kusema kweli nilianza kuifanyia kazi taarifa hiyo na ninatarajia ifikapo Ijumaa
nitakamilisha kazi hiyo.”
Kwa upande wake, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Alphonce Gagambobyaki
alisema hadi sasa ofisi yake haijafahamu nani aliyempa mkuu wa mkoa taarifa ya
ukaguzi wa wafanyakazi hewa kwa sababu taarifa aliyonayo mezani haijasainiwa.
“Kuna tatizo la ofisi hii kukaimiwa na
zaidi ya watu wanne tangu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Dalikunda Kimulika
alipostaafu Februari. Ni vigumu kujua nani alihusika nayo bila kuona saini,” alisema Bagambobyaki.
Alisema taarifa hiyo inaonekana haikusainiwa kutokana na hofu baada ya watumishi waliobainika kutokuwapo kwenye vituo vyao vya kazi karibu wote kuonekana kuwa na ruhusa maalumu.
Alisema taarifa hiyo inaonekana haikusainiwa kutokana na hofu baada ya watumishi waliobainika kutokuwapo kwenye vituo vyao vya kazi karibu wote kuonekana kuwa na ruhusa maalumu.
“Wakati bado tunajiridhisha kujua ni ruhusa ya aina gani na hawa
watumishi wako wapi, ndipo taarifa ilipotangazwa kwamba mkoa hauna watumishi
hewa,” alisema.
Hata hivyo, alisema anaamini taarifa sahihi itajulikana baada ya timu maalumu iliyotoka Tamisemi kukamilisha uhakiki wilayani humo jana.
Hata hivyo, alisema anaamini taarifa sahihi itajulikana baada ya timu maalumu iliyotoka Tamisemi kukamilisha uhakiki wilayani humo jana.
“Timu ile ya Tamisemi imekwenda mbele zaidi katika uhakiki wake kwa
kukagua mtumishi mmoja mmoja hadi vijijini na imekamilisha kazi yake jana,” alisema Bagambobyaki.
Kuhusu iwapo aliyekuwa mkuu wa mkoa alitumia taarifa zao au la? kaimu mkurugenzi huyo alisema: “Iwapo RC alitumia taarifa zetu au la, hilo siwezi kulisemea kwa sasa.”
Kuhusu iwapo aliyekuwa mkuu wa mkoa alitumia taarifa zao au la? kaimu mkurugenzi huyo alisema: “Iwapo RC alitumia taarifa zetu au la, hilo siwezi kulisemea kwa sasa.”
Kilango ambaye juzi
alisema hakuwa amepata taarifa hivyo asingeweza kuzungumzia kutenguliwa kwake,
jana alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kabisa na Dachi akaeleza kuwa
ameupokea uamuzi huo kwa kuwa Rais ndiye mteule wake.
Taarifa ya kutenguliwa
kwa watumishi hao wa umma sasa imekuwa kaa la moto kwa wakuu wa wilaya makatibu
tawala wao, na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za mkoa huo.
Alipoulizwa kuhusu
taarifa hizo za watumishi hewa, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro
alisema hawezi kuzungumzia lolote.
“Sisemi lolote na wala sizungumziii mkoa,” alisema na kukata simu ambayo haikupokewa tena.
Kama ilivyokuwa kwa mkuu wake wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aligoma kuzungumzia uwezekano wa halmashauri yake kutoa taarifa zilizompotosha Kilango.
Kama ilivyokuwa kwa mkuu wake wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aligoma kuzungumzia uwezekano wa halmashauri yake kutoa taarifa zilizompotosha Kilango.
“Sitaki kulizungumzia hilo, nawaachia
wanaolijua walizungumzie,”alisema Kalinjuna.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa alikata simu yake mara kadhaa alipopigiwa na baadaye kutuma ujumbe mfupi wa maneno akisema yuko kwenye kikao na kuelekeza atumiwe ujumbe ambao hata alipotumiwa hakujibu.

No comments:
Post a Comment