Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa
inaboresha huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya Geita ikiwa ni pamoja
na kuipatia hadhi ya kuwa hospitali ya mkoa.
Akiuliza swali la nyongeza katika kipindi cha
maswali na majibu Bungeni Dodoma, Mbunge wa Geita mjini Mh.Constatine Kanyasu,
alitaka kujua kuwa ni lini watumishi wa afya pamoja na madaktari watapelekwa
katika hosptali hiyo.
akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa nchi ofisi
ya Raisi Tamisemi, Naibu Waziri Tamisemi Suleman Jafo pamoja na kuwapongeza
wabunge wote wa Geita kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa (GGM) kwa kazi waliyoifanya
amesema kuwa muda si mrefu Wizara ya afya itatoa idadi ya waajiriwa wakati huo
hospitali ya wilaya ya Geita ikipewa kipaumbele kwa sababu ina hadhi ya
kutosha.
Hata hivyo Mhe.Jaffo amesema kuwa katika bajeti ya
mwaka huu Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika halmashauri zote nchini
ikiwa ni pamoja na kuboresha vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali
za mkoa.
No comments:
Post a Comment