Umoja wa Wazazi Mkoani Geita umetoa tamko la kuunga mkono
juhudi za dhati zinazofanywa na Rais Joseph Magufuli la kulikomboa Taifa la
Tanzania litakaloweza kusimama na kujiongoza kwa kuwa na watendaji wanaoendana
na kasi ya Rais.
Umoja huo umetoa tamko hilo wakati wa kuadhimisha kilele
cha wazazi mkoani Geita na kuandaa ibada ya kumuombea raisi Maggufuli na nchi
kwa ujumla.
Umoja huo umesema kwa muda mfupi
usimamizi katika mapato ya serikali yamefanikiwa kwa kuziba mianya ya ukwepaji
kodi na wana imani kubwa mapato ya taifa yatazidi kupanda na kuondokana na
utegemezi.
Kutokana na uongozi mzuri wa awamu ya tano wanaamini
mabadiliko yatazidi kuonekana na sifa za viongozi bora zitaonekana.
Katika hatua nyingine wamesema baadhi ya viongozi wa
mataifa ya nje yamedaiwa hayawezi kumuunga mkono kiongozi wa Afrika anayefanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment