Friday, 15 April 2016

WANANCHI WALALAMIKIA HUDUMA DUNI ZINAZOTOLEWA NA ZAHANATI YA KATA YA MATENDO MKOANI KIGOMA

Wananchi wa kata ya Matendo , mkoani na wilayani Kigoma wamelalamikia huduma zisizoridhisha  za  afya zinazotolewazo na zahanati ya kata hiyo, hivyo wamemwomba diwani kushughulikia kero hizo.


Wananchi hao wametoa malalamiko  yao  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mayange, ambapo  wamesema  huduma zisizoridhisha  zimekuwepo kwa muda mrefu huku akina mama wakiwa ni wahanga wakubwa  wakati  wa kupata matibabu.

Mbali na changamoto  za afya pia wananchi hao wamehoji  matumizi mabaya ya fedha  za wananchi  ambapo  wameeleza zaidi kero zao.

Akijibu  kero hizo diwani wa kata   ya   Matendo, Athumani Ntanyagara, amesema kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana, aliahidi kuwa atasimamia shughuli zote za miradi ya maendeleo  na kulinda haki za wananchi wa kata hiyo.

Katika hatua nyingine amewahakikishia wananchi kufuatilia  sakata  la ubadhirifu  wa fedha lililoibuliwa  kwen
ye mkutano huo

No comments:

Post a Comment