Wafugaji wilayani Bukombe Mkoani Geita walalamika juu ya unyanyasaji na mateso
wanayofanyiwa na askari wa pori la akiba la kigosi muyowosi kwa kwa kupigwa
viboko,kutozwa faini zisizo na risiti na kutishiwa kupigwa risasi kutokana na
kufuga mifugo yao katika pori hilo.
Wakizungumza mbele ya mawaziri wa maliasili na utalii
Jumanne Maghembe na waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba wamedai
kuna wenzao wameshapoteza maisha na mifugo mingi kupigwa risasi na kuwaacha
baadhi ya wafugaji katika wimbi la umasikini.
aidha wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya malisho na
tayari yaliyotengwa yanatumiwa na wakulima na mengine ni makazi ya watu.baadhi
ya wafugaji wanaelezea kuwa wamekuwa na kilio hiki kwa muda mrefu na kudai
wameshafanyia vikao vingi na viongozi wa serikali lakini muafaka wa kudumu
haujapatikana.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Serikali wanadaiwa kuwa
chanzo cha matatizo yanayotokea huku Mbuge wa Bukombe Dotto Biteko anadaiwa
kutumiwa na wafugaji.
Katika pori la muyowosi kuna ng`ombe zaidi ya milioni
mbili na serikali ipo katika mpango wa kutafuta maeneo,katika hatua nyingine
wafugaji wamepewa muda kufikia june 15 wawe wameondoka katika pori hilo hata
hivyo chama cha wafugaji kanda ya ziwa kimeomba kupata suluhu ya kudumu ili
wafugaji wajikite katika kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment