Serikali imekiri kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa
watu katika magereza huku sababu ikielezwa ni ucheleweshwaji wa kesi unaosababishwa
na kucheleweshwa kwa kesi za baadhi ya
washitakiwa.
Akizungumza na watendaji wa Serikali mkoani Geita
katika ofisi za mkuu wa mkoa,Waziri wa katiba na sheria, Dkt. Herson Mwakyembe amesema
kuwa kutokana na kucheleweshwa kwa kesi
hali hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa mlundikanao mkubwa wa watu hali
ambayo imeendelea kutishia usalama
wa afya kwa baadhi ya wafungwa.
Akitoa taarifa ya Wkoa kwa Waziri Mwakyembe Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mh.Manzie Manguchie amesema kuwa
mkoa wa Geita unakabiliwa na uhaba wa gereza la mkoa hali ambayo kumekuwa na
changamoto ya watu kuwa wengi katika
magereza.
Aidha waziri Mwakyembe amewata wananchi mkoani hapa
kubadilika na kuachana na vitendo vya imani za kishirikina za mauaji dhidi ya
watu wenye ulemavu wa ngozi (zeruzeru) huku akiitaja mikoa ya Mwanza,Mara
na Geita kuongoza kwa mauaji hayo.
Waziri Mwakyembe amefika asubuhi na mapema leo
akitokea jijini Mwanza na yupo mkoani Geita
kwa ziara ya siku moja ambapo atatembelea,Ofisi
ya Mwanasheria mkuu,Ofisi ya vizazi na vifo (RITA) na kuzungumza na wafungwa katika gereza la wilaya ya Geita.
No comments:
Post a Comment