Wananchi waishio mtaa wa Mgusu wilayani na mkoani Geita wametakiwa kujua kuwa wanaishi katika sehemu ya leseni ya utafiti wa Mgodi
wa Dhahabu wa Geita( GGM) na kwamba eneo
hilo bado mgodi haujaona sababu ya
kulichukua.
Akiuliza swali
katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge
wa viti maalum CHADEMA mkoani hapa Upendo
Peneza, ametaka kujua kuwa serikali inaweka msukumo gani kwa mgodi kuhakikisha kuwa
inawalipa wananchi fidia ili waweze kuondoka katika maeneo hayo.
Akijibu swali la mbunge
wa viti maalum,mkoani hapa Naibu Waziri
wa nishati na madini Dkt.Merdad Kalemani amesema kuwa kwa sasa hivi eneo hilo
bado halijaanza kutumika na kwamba mgodi hauoni sababu ya kulichukua .
Katika hatua nyingine
pia wananchi mkoani hapa wamekuwa na maoni tofauti juu ya bunge la bajeti ya
mwaka 2016/17 lililoanza rasimi hii leo mkoani dodoma.
No comments:
Post a Comment