Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya
kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala hao
wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha
wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi
lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala
walioapishwa ni;
- Arusha
- Richard Kwitega
- Geita
-
Selestine Muhochi Gesimba
- Kagera
- Armatus C. Msole
- Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
- Pwani - Zuberi Mhina
Samataba
- Shinyanga - Albert
Gabriel Msovela
- Singida
- Dr. Angelina Mageni
Lutambi
- Simiyu
- Jumanne Abdallah
Sagini
- Tabora
- Dkt. Thea Medard Ntara
- Tanga
- Eng. Zena
Said
Makatibu Tawala
wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi
na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula
kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa
Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016
No comments:
Post a Comment