Umoja wa waganga wa
tiba asili wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita
umempongeza mkuu wa wilaya mh Ibrahim Marwa, kwa kutoa ushirikiano ambao
umesaidia kupunguza kasi ya mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi.
Akitoa taarifa hiyo
katika mkutano wa waganga wa tiba asilia wilayani humo mwenyekiti wa umoja
huo kanda ya ziwa Bujukano John Mahungu
amesema kuwa ushirikiano uliokuwepo kati ya umoja huo na uongozi wa wilaya umefanikisha
kupunguza mauaji kutoka asilimia 80% mwaka 2014 hadi kufikia 10% hivi sasa.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale
mh Ibrahim Marwa ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika mkutano huo ,amesema
kuwa kwa
sasa wilaya yake imedhamiria kushirikiana na viongozi wa vijiji kukusanya
takwimu za wazee ikiwa ni moja kati ya njia za kudhibiti wimbi la mauaji.
Aidha Marwa ameushukuru
uongozi wa waganga wa tiba asilia
kwa kutoa elimu kwa waganga waliotoka
maeneo ya vijijini ikiwa ni
pamoja na ulinzi shirikishi hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mauaji katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment