Naibu
Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Faustine Ndugulile (kulia) akiongea wakati anazindua Bodi Tendaji ya kwanza ya
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Jengo la Mkemia, Dar es Salaam. Kushoto (waliokaa) ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Profesa Esther Hellen Jason na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.
Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia) akitoa hotuba wakati wa
uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali ambayo ilizinduliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kutoka kushoto
waliokaa) kwenye ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es
Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Otilia Gowele (aliyesimama)
akiongea kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kutoa
hotuba na kuzindua rasmi Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali leo kwenye Ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali.
Naibu Waziri Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile
(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (wa pili kulia) Sheria na
kanuni zake zinazosimamiwa na Mamlaka ikiwa ni ishara ya kuizindua rasmi Bodi
hiyo. Wengine katika picha ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Otilia
Gowele (mwenye koti jeupe) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko
(wa kwanza kulia).
Mameneja
na wakuu wa Vitengo wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka hiyo ambayo
imezinduliwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile leo kwenye ofisi za Mkemia Mkuu wa
Serikali, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akiwa pamoja na
Wajumbe wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali pamoja na Kaimu Katibu Mkuu (Afya), Dkt. Otilia Gowele (wa pili kutoka
kushoto) na Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Bi. Tunu Temu( wa kwanza
kushoto).
Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGLA) imetakiwa kuandaa
mkataba wa utoaji huduma ili kuepuka ucheleweshaji katika utoaji wa majibu kwa
wananchi wanaohitaji huduma za mamlaka hiyo.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo yenye jumla
ya wajumbe saba.
"Mamlaka hii ni
nyeti sana kwa hiyo tunatakiwa kuwa na mkataba wa utoaji wa huduma ili mtu
akileta sampuli zake hapa afahamu lini atapata majibu hivyo kujiondoa kuwa
sehemu ya ucheleweshaji wa utoaji wa haki," alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,Dkt. Ndugulile
ameongeza kuwa ni lazima kuwa na ithibati kutokana na umuhimu wa Mamlaka hiyo
kwani imepewa jukumu la kisheria kusimama Mahakamani kutoa majibu sahihi juu ya
uchunguzi fulani hivyo ni lazima apatikane mtu wa kusimamia ubora ili majibu
yanayotolewa yawe yanaaminika na kuweza kutumika ndani na nje ya nchi.
Naibu Waziri huyo
amefafanua kuwa Mamlaka imepata sheria mpya, muundo mpya, uongozi mpya pamoja
na bodi mpya, hivyo imepewa meno ya kisheria katika kutekeleza majukumu yao
kikamilifu pamoja na kutatua changamoto zilizopo.
Kwa upande wake Mkemia
Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko ameiomba Serikali kutatua baadhi ya
changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo zikiwemo za upungufu wa watumishi 172
pamoja na kununua mitambo ya kisasa kwani mitambo iliyopo haiendani na hali
halisi.
Vile vile amemuahidi
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ataendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali
ikiwemo suala la kuhamia jijini Dodoma.
Naye Mwenyekiti wa Bodi
hiyo, Prof. Esther Hellen Jason amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua katika
nafasi hiyo ambapo amesema bodi itafanya kazi kwa weledi na kujituma ili
kufikia matarajio ya nchi kama yalivyopangwa.
No comments:
Post a Comment