Mkulima wa mpunga kutoka kijiji cha
Nyawilimelwa Bw Lazaro Lujina akizungumza juu ya hataua ya wao kuendelea kuhuza
mazao yao kwa bei ya hasara.
Baadhi ya magunia ya Mpunga yakiwa kwenye ghara la kuhifadhia mazao hayo. |
Bw. Rashid Kibashala akizungumza juu ya
hatua ya kuendelea kununua kwa bei za chini na wao kuhuza bei ya Juu
Ngunia ambalo wakulima wamekuwa wakililalamikia kuwa limekuwa likiwasababishia hasara kutokana na ujazo wake ulivyo. |
Wakulima wa Mpunga kijiji cha Nyawilimelwa Wilayani Geita Mkoani humo wameiomba Serikali kuwatengenezea Soko la pamoja ambalo litasaidia kuuza mazao yao kwa bei nzuri zaidi kuliko sasa hivi ambavyo wamekuwa wakiuza bei ya hasara kwa walanguzi wanaoingia kijijini Humo.
Wakizungumza mtandao
huu Kijijini hapo baadhi ya wakulima wamesema kukosekana kwa soko nzuri la
kuhuzia mazao yao imekuwa ni sababu ya wao kuhuza kwa bei isiyo
nzuri na pindi wanapotaka kupereka mjini wamekuwa wakikutana na changamoto ya
ubovu wa Barabara.
“Tatizo ni kukosekana
kwa soko ndio sababu ambayo imekuwa ikisababisha sisi wakulima kushindwa kukaa
na mazao kwa muda mrefu ndani na unakuta na sisi tunashida nadhani serikali
ingeona umuhimu ikatutengenezea soko ingependeza zaidi kama vile pamba tunaona
inasoko lakini mpunga hauna soko kabisa” Alisema Julius Mandegere.
Kutokana na malalamiko
ya wakulima kunyonywa na baadhi ya walanguzi mtandao imezungumza na Mlanguzi wa
mazao hayo,Bw Rashid Kibashala ambapo amesema mala nyingi wamekuwa
wakifanya maelewano kabla ya biashara.
“Kila biashara
inamaelewano hivyo sisi tunafanya maelewano na wakulima juu ya bidhaa ambayo
tunanunua kwa lengo la kwenda kupata faida siunajua kaka na sisi tunasafirisha
hivyo tunaitaji faida sisi hatuwanyonyi” Alisema Kibashala.
Mwenyekiti wa Kijiji
hicho,Bw Majuto Mariatabu amesema hili kuwasaidia wakulima kutokuuza mazao yao
holela wamekuwa wakiwakamata wale ambao wameendelea kuwagalaliza wakulima hao.
Afisa Kilimo wa Mji wa
Geita,Bw Samweli Ng’wandu akielezea namna ambavyo wametoa elimu kwa
wakulima juu ya umuhimu wa utunzaji wa chakula hususani katika kipindi hiki cha
mavuno.
No comments:
Post a Comment