Friday 10 November 2017

SERIKALI KUAJIRI MAAFISA UGANI 1,487



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. George  Mkuchika 

Serikali imepanga kuajiri maafisa Ugani 1,487 katika mwaka wa Fedha 2017/2018 ili kuziba pengo la upungufu wa wataalamu hao kote nchini na kuongeza tija katika uzalishaji kwenye sekta ya Kilimo.

Akijibu swali la mbunge wa Nanyamba Mhe. Abdalla Chikota wakati wa Kipindi cha maswali  na majibu  Bungeni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. George  Mkuchika amesema kuwa kati ya mwaka 2013/2014 hadi 2016/2017 jumla ya Maafisa Ugani 5,710 waliajiriwa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

“Serikali imekuwa ikitoa vibali vya ajira za Maafisa Ugani katika Mamlaka za Serikali ya Mitaa kila mwaka wa fedha kutegemea uwezo wa bajeti” Alisisitiza Mkuchika.

Akisisitiza  Mhe.  Mkuchika amesema kuwa Serikali inatambua upungufu wa Maafisa Ugani hasa katika Halmashauri mpya  na Miji na itahakikisha inawapeleka Maafisa hao ili kuleta uwiano kati ya Halmashuri Kongwe na zile mpya.

Aliongeza kuwa Wizara yake itashirikiana na Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa udahili katika vyuo vya Ugani unaongezeka ili idadi ya wataalamu hao iongezeka kulingana na mahitaji.

Katika Kukuza na kuongeza tija Katika Sekta ya Kilimo  Serikali imeweka mkazo katika kuongeza ujuzi na maarifa 

No comments:

Post a Comment