Translate message
Turn off for: Swahili
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafari hayo akiongozana na mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Senga wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Mahabara shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikagua ujenzi wa vyoo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi pamoja na Mkuu wa shule ya Senga ,wakielekea kwenye madarasa ambayo yametengwa kwaajili ya wanafunzi kulala shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikagua sehemu ya wanafunzi ambayo wanalala.
Eneo ambalo wanafunzi wamekuwa wakitumia kulala ambao ni wavulana.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiwa kwenye chumba ambacho kinatumika kama mahabara na hapa anaelezewa na mwanafunzi namna ambavyo mapigo ya moyo yanafanya kazi mwilini.
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Senga Mwl,Magoma Komesi Magero akiwatambulisha baadhi ya wageni waalikwa.
Walimu wa shule ya Sekondari ya Senga wakijitambulisha mbele ya Mgeni rasmi.
Wazazi wakiwa kwenye mahafari.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wanafunzi kujisomea kwa bidii. Mkuu wa wilaya ya Geita akiwa kwenye picha ya pamoja na Walimu wa shule ya sekondari Senga.
PICHA NA JOEL MADUKA
Ukosefu wa walimu
wa sayansi imeelezwa
kuwa ni kikwazo ambacho
kimesababisha wanafunzi wengi
kutokuwa na mwamko wa masomo hayo
na kujikuta wengi wao wakikimbilia kwenye
masomo ya sanaa.
Hayo yamebainishwa na
mwalimu wa shule ya sekondari ya Senga
Mwl,Magoma Komesi Magero kwenye mahafali
ya nne,amesema pamoja
na shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya Kitaifa na
mtihani wa utimilifu bado inakabiliwa na
changamoto ya walimu
wa masomo ya Baioloji na kemia.
Akisoma Risala kwa mgeni rasmi ambayo iliandaliwa na
wanafunzi wa Kidato cha nne, Venasia Frances Amesema shule hiyo inawalimu wa masomo ya sayansi
watano tu ukilinganisha na idadi ya wanafunzi ambao wapo shuleni hapo huku
akigusia na swala la vyumba vya madarasa.
Mgeni rasmi kwenye
mahafali ,Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi,ameitaka halmashauri
kuongezea walimu wa masomo ya sayansi na pia amewapongeza walimu hao watano wa
masomo ya sayansia pamoja na uchache wao wamejitahidi kufanya vizuri kwenye
masomo hayo.
Jumla ya
wanafunzi ambao wamesajiliwa
kufanya mtihani kwenye shule ya sekondari ya Senga
ni 97.
No comments:
Post a Comment