Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga. |
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi. |
Wananchi wa kijiji cha Kazibizyo wakishiriki kusomba mawe. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiendelea na harakati za kushiriki ujenzi wa zahanati kijijini hapo. |
Wakina mama wakishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati kijiji cha Kazibizyo |
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akizungumza na wananchi wa kijiji hicho juu ya kujitolea kwenye swala la maendeleo bila ya kutegemea serikali. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazibizyobaada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo.
|
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji
cha Kazibizyo na Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea maendeleo
ya vijiji vyao.
Mhandisi Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati
kwenye Kata ya Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea
wananchi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo
Alisema matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika
badala yake kuweka mbele maslahi binafsi.
“Shida kubwa wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na
viongozi bora viongozi sio viongozi bora viongozi ambao awawezi
kuamasisha viongozi ambao kazi yao ni kula michango ya wananchi
viongozi ambao fedha zikija wanaangalia kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale
makombo ambayo yanajenga vitu vibovu vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo
hatuwezi kuwavumilia Geita,ni bora wafungashe virago watafute Mikoa
mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama unaona kazi ni ngumu achia bodi” Alisisitiza
Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi alisema wananchi ndio nguzo kubwa ya maendeleo kwenye
maeneo yao hivyo lazima wawe na afya bora na elimu ili wafanya kazi za
maendeleo.
Mmoja wa wananchi Bi Sophia Sangizo alielezea wamekuwa
wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kusababisha wanawake wengi
kujifungulia nyumbani hali ambayo imekuwa ikisababisha matatizo kwao.
Kwa upande wa Mzee Mayoke Ambrose Maziku ambaye ametoa kiwanja kwaajili
ya ujenzi wa zahanati kijijini hapo alisema kuwa msukumo mkubwa ambao
umepelekea kutoa kiwanja ni kutokana na mwaka 2013 na 2007 alipoteza watoto
wake kutokana na kukumbwa na umauti sababu kubwa ikiwa ni kuwa mbali na huduma
za afya kwani wamekuwa wakitembea umbali wa kilomita 20 kufuata huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment