Mhandisi Robert Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Mkoa na Wilaya Geita na kamati ya usalama ya Mkoa wakikagua miundombinu ya shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Halmashauri ya Mji Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita(Wakwanza kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nguzombili wakati wa ziara yake katika Shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiingia ndani ya moja ya darasa lililojenjwa chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya Msingi Nguzo Mbili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita Mhandisi Modest Apolinary akifafanua jambo kuhusu utekelezaji miradi ya lipa kwa matokeo kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara yake shule ya msingi Nguzombili iliyopo Halmashauri ya Mji Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya
Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa
vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili.
" Inashangaza
sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni
katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na
nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya Serikali" Alisema Lughumbi.
Akiwa shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia
vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa
madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye
fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii.
Katika hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa
Shule ya Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa miundombinu
hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka.
Aidha, ameagiza shule hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo
vilivyojengwa vianze kutumika badala ya kufungwa.Pamoja na kutembelea Shule ya
Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea shule ya Sekondari na kukagua
ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa
matokeo.
Shule ya Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia
shilingi milioni 13 kwa kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya
kisasa pamoja na ukarabati wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na
fedha iliyobaki katika bajeti ya darasa moja.
No comments:
Post a Comment