Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema leo bungeni ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Spika Job Ndugai lililotaka serikali kutoa
kauli kuhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutakiwa kutoa fedha ili wasajiliwe
kabla ya kupata mikopo.
Agizo la Spika
lilitokana na Mwongozo uliombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata
ambaye alieleza bunge kuwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika vyuoni baada ya
kutakiwa walipe fedha za usajili kabla ya kupewa mkopo.
"Serikali
imeshawaagiza wakuu wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa
fedha kwa wanufaika kwa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali,"
amesema.
Amesema inasikitisha
sana kuona baadhi ya vyuo vinadiriki hata kuwakataa wanafunzi waliowadahili wao
wenyewe au vinawalazimisha wachukue programu tofauti na walizokuwa
wamechaguliwa awali na vyuo husika.
" Jambo
hili halikubaliki hata kidogo na linaleta shaka kuhusu uadilifu wa vyuo husika.
Naiagiza TCU (Tume ya Vyuo Vikuu) na Kurugenzi ya Elimu ya Juu ya Wizara,
kufuatilia kwa karibu mambo yote yanayopendelea vyuoni wakati wanafunzi
wanaripoti na kubainisha wote wanaokiuka taratibu na kuwanyima wanafunzi haki
yao ya kusoma programu wanazoitaka," amesema.
Amesema Serikali
haitasita kuchukua hatua kali kwa vyuo vyote vitakavyoleta usumbufu usio wa
lazima kwa wanafunzi na kuwafanya wapoteze muda ambao wanapaswa kuutumia kwa
masomo.
No comments:
Post a Comment