Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma cha Kiwango cha
Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza
miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na udhibiti wa ubora wa chakula na dawa
katika ukanda wa Afrika Masharika kutunikiwa cheti hicho.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akielezea
jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma
cha Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es Salaam. TFDA
imekuwa ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na udhibiti wa ubora wa
chakula na dawa katika ukanda wa Afrika Masharika kutunikiwa cheti hicho.
Mkurugenzi
wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Prof. Egid Mubofu akielezea jambo wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma cha Kiwango
cha Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza
miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na udhibiti wa ubora wa chakula na dawa
katika ukanda wa Afrika Masharika kutunikiwa cheti hicho.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine
Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki
Ubora wa Huduma cha Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es
Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na
udhibiti wa ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa Afrika Masharika
kutunikiwa cheti hicho. Kutoka kuhoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFDA
Dkt. Ben Moses, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo na Kaimu Meneja Uhakiki
Mifumo wa TFDA Sunday Kisoma.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine
Ndugulile wakiwa wameshika Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma cha
Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo
Jijini Dar es Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza miongoni mwa mamlaka
zinazoshughulika na udhibiti wa ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa
Afrika Masharika kutunikiwa cheti hicho. Kutoka kuhoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
TBS, Prof. Egid Mubofu, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TFDA Dkt. Ben Moses, Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo na Kaimu Meneja Uhakiki Mifumo wa TFDA Sunday
Kisoma.
Akzungumza katika uzinduzi wa Cheti
hicho leo Jijini Dar es Salaam, Dkt Ndugulile
alisema cheti hicho cha ubora ni kielelezo cha Taasisi hiyo kusimamia misingi
ya ubora katika utendaji kazi wake katika Mfumo wa uhakiki ubora wa huduma katika
kiwango cha Kimataifa.
Ðk. Ndugulile amesema kuwa mafanikio
hayo ya TFDA ni matokeo ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
katika kuhakikisha huduma bora za afya hususani katika udhibiti na upatikanaji
wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
“Utekelezaji wa mfumo huu na kupatikana
kwa cheti hiki ni ishara nzuri kwamba TFDA inasimamia vyema mifumo yake ya
kiutendaji ili kuhakikisha huduma zitolewazo zina ubora na zinakidhi matakwa ya
kiwango cha Kimataifa cha ISO 900: 2015, hii pia inaleta imani kubwa kwa sisi
tunaowasimamia utendaji wenu na wananchi wanaotumia bidhaa mnazozidhibiti kwa
ujumla,” Alisema Dkt. Ndugulile.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti
Sillo alisema mamlaka hiyo imetunukiwa cheti hicho kimeifanya taasisi hiyo kuwa
Mamlaka ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazojihusisha na udhibiti wa ubora wa
chakula na dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki na ya pili kwa nchi za Kusini
mwa Jangwa la Sahara.
Aliongeza kuwa TFDA imekuwa ikitekeleza
Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma kuanzia mwaka 2005 baada ya kufanya tathmini
ya namna bora ya kufanya shughuli za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora
kwa wateja.
“Katika kuendelea kukidhi matarajio ya
wateja na kuendana na matakwa ya wateja wetu na wadau kwa ujumla, tuliamu
kuboresha Mfumo wetu wa Uhakiki Ubora wa Huduma ili uendane na matakwa ya
kiwango kipya cha Kimataifa, tulifanikiwa kutunukiwa cheti cha ISO 9001:2015
baada ya ukaguzi wa kina mnamo mwezi Agosti mwaka huu,” alisema Mkurugenzi
Sillo.
No comments:
Post a Comment