Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (Kulia) akiwa na Aliyekuwa Makamu wake Emmerson Mnangagwa
Rais Mugabe
alimtangaza Mnangagwa kuwa ni adui wa Serikali yake akidai kuwa alikuwa
anapanga njama za kushika dola.
“Alienda kwa nabii
kanisani ili aambiwe Mugabe atakufa lini. Lakini aliambiwa angekufa yeye
kwanza,” Mugabe aliwaambia waandishi wa habari Jumatano alipotangaza kumtumbua
Mnangagwa.
Rais Mugabe aliongeza
kuwa walikuwa wakifuatilia mienendo yake kwa muda mrefu na njama alizokuwa
akipanga kushika dola bila kufuata utaratibu wa chama na kwamba wameona
wamuondoe yeye lakini wale aliokuwa akishirikiana nao watajua namna ya kuishi
nao wakiwa ndani ya chama cha ZANU-PF.
Mke wa Rais Mugabe,
Grace Mugabe anatajwa zaidi kuwa ndiye atayechukua nafasi ya Makamu wa Rais
huku ikielezwa kuwa ni sehemu ya kumtengenezea njia ya kurithi nafasi ya
mumewe.
Mama Grace amekuwa na
uadui mkubwa na Mnangagwa akimtaja kuwa ni msaliti. Pia, alimfananisha na nyoka
ambaye alidai anapaswa kuondolewa mapema.
Hata hivyo, tamko
lililotolewa na watu wa karibu wa Mnangagwa limekanusha kuwa alikuwa na njama
zozote dhidi ya Serikali hiyo na kwamba amekuwa mwaminifu wakati wote kwa Rais
Mugabe.
No comments:
Post a Comment