Afisa Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji
akizungumza katika mkutano wa Global Business Forum 2017 kuhusu Viwanda kwa
Nchi za Afrika, mkutano huo wa siku mbili umefanyika Dubai, UAE na kuhudhuriwa
na watu 5860 wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na
wafanyabiashara.
Dewji ametoa pongezi
hizo wakati akizungumza katika mkutano wa siku mbili wa Global Business Forum
2017 (GBF) kuhusu Viwanda kwa Nchi za Afrika uliofanyika Dubai, Falme za
Kiarabu (UAE).
Mfanyabiashara huyo
ambaye anamiliki viwanda 41 alisema uamuzi aliochukua Rais Magufuli ni mzuri
hasa katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati.
Dewji alisema kampuni
yake ya MeTL Group itaendelea kushirikiana na serikali na katika kipindi cha
miaka kadhaa ijayo amejipanga kuhakikisha anatoa ajira kwa
Watanzania 100,000 jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa nchi na kwa
wananchi..
“Nianze
kwa kumpongeza Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa shabaha yake ya viwanda, ni
nzuri sababu kuna ongezeko la thamani lakini pia watu wanaweza kupata ajira na
pia hizi biashara zitalipa kodi ambazo zitaisaidia serikali kuwekeza kwenye
mambo ya afya na maji na huduma za jamii. Mimi shabaha yangu kwenye miaka saba
au nane ijayo MeTL Group tunataka tuajiri watu 100,000,” alisema Dewji.
Dewji ambaye kwa mujibu
wa jarida la Forbes ni tajiri namba moja nchini aliongeza kuwa utendaji wa Rais
Magufuli ni wa kasi hivyo anategemea kuwa katika kipindi cha miaka michache
ijayo uchumi wa Tanzania utakuwa umekuwa sana.
“Mimi naona kwa kasi ya
Mhe. Rais kwenye miaka miwili au mitatu ijayo tutakuwa tumefika mbali sana,
uchumi wetu kwasasa ni asilimia sita au saba lakini kama tukitaka kuondoa
umaskini lazima nchi yetu ukuaji wa uchumi uanze kukua kwa zaidi ya asimilia
10, mimi nina muamini sana Mhe. Rais na shabaha yake kwahiyo Mungu atutangulie na
sisi tupo nyuma yake tutafika hivi karibuni,” alisema Dewji.
Pia Dewji alizungumzia
umuhimu wa mkutano wa GBF ambao umekutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali ya
Afrika wakiwepo viongozi wa serikali za nchi za Afrika na wawekezaji alisema ni
nafasi ya kipekee kwani pamoja na kujadili viwanda pia amepata nafasi ya
kuwaelezea washiriki wa mkutano fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini.
“Umuhimu ni mkubwa sana
nakuja hapa kama MO lakini pia nawakilisha nchi yangu Tanzania, nimeitangaza
nchi yangu ili watu waje na wawekeze, nimewaeleza mazingira yetu ya uwekezaji
ni mazuri, tuna malighafi na tunahitaji viwanda angalau watu wetu wa Tanzania
wapate ajira na serikali ipate kodi,” aliongeza Dewji.
No comments:
Post a Comment