Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl
Herman Kapufi akisisitiza wafanyabiashara kutokubuguziwa na mtu yoyote kwenye
shughuli zao wakati wa kikao hicho cha baraza.
(Katikati)
ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita ,Leornad Kiganga
Bugomola,akifuatiwa(kulia) na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Mhandisi Modest
Aporinal pamoja na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Costantine Molandi
wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Baadhi ya madiwani wakiwa
kwenye kikao hicho
Serikali Wilayani Geita imesema kuwa mfanyabiashara
anayehitaji kuwekeza kwenye biashara ya kuuza nyama kwa bei nafuu anaruhusiwa
kufanya biashara hiyo sawa na watu wengine bila ya kubughudhiwa na mtu ama
kikundi chochote.
Hatua hiyo imekuja kutokana na mfanyabiashara ambaye jina lake halijafahamika
mara moja kufungua duka la nyama na kuuza kwa Sh,3500 kwa kilo kuambiwa na
umoja wa wamiliki wa maduka ya nyama kuwa afunge kwa kuwa wao wamekuwa wakiuza
kwa Sh 6000 kwa kilo moja.
Amedaiwa kuwa anauza nyama kwa bei ambayo haijazoeleka mjini Geita na
kwamba bei hiyo imezoeleka kwenye Kata ya Kasamwa .
Akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Mji wa
Geita,Mwenyekiti wa halmashauri ya hiyo Bw, Leornad Bugomola alisema
kumekuwa na kikundi kinachopanga bei ya nyama mjini humo na hivyo kusababisha
kumtoa mwekezaji aliyekuwa akiuza nyama kwa bei ya chini.
“Mkuu wa wilaya kutokana na watu
kuhangaika kufuata nyama Kasamwa sisi tulionelea tumuombe mtu aje
afungue Bucha ambayo itakuwa na Bei nafuu hivyo alikubali lakini kimezuka kikundi
ambacho kimekuwa kikimpinga muwekezaji huyu na kwamba afunge bucha yake
kutokana na wao kutokuafiki bei hiyo ili swala nimeona nikwambie ili uweze
kulishughulikia” Alisema Bugomola
Kutokana na maombi hayo mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman
Kapufi alisema katika wilaya anayoiongoza anataka kitu bora na kwamba suala la
bei haliwezi kuwafanya watu kutowekeza kwenye wilaya yake na kama kuna watu
wengine ambao wanauza bei nafuu ya nyama ni vyema wakapatiwa maeneo ya biashara
hiyo kwani hakuna mtu ambaye anaweza kuingilia biashara ya mtu mwingine.
Baadhi ya wakazi wa mjini Geita wamepongeza uamuzi huo wa serikali kwa
kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu bei ya nyama ya sasa.
No comments:
Post a Comment