Sunday 5 November 2017

"KUKAMILIKA UWANJA WA NDEGE MKOANI GEITA KUTAFUNGUA FURSA ZA UCHUMI" - PROF. MBARAWA

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa waGeita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3,
unajengwa na makandarasi wazalendo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya watendaji wakati alipokuwa anawasili kwenye viwanja vya hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege Wilayani Chato Mkoani Geita.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato na Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakicheza na kwaya ya Mwagasege wakati wa Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa uwanja wa ndege.

Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarembe akiwatambulisha wageni mbali mbali ambao wameuzulia kwenye hafla hiyo Wilayani Humo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akitoa taarifa ya Mkoa kwa niaba ya wananchi Mkoani humo na kwamba kiwanja hicho kitakapo kamilika kitaweza kufungua milango ya fursa mbali mbali ndani ya Mkoa huo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Geita.

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini.Costatine Kanyasu akisalimia wananchi wakati wa wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye
sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Doto Mashaka Biteko akitoa salaamu za Jimbo lake kwa Mgeni rasmi na wananchi ambao walikuwa wamekusanyika kwenye viwanja  hivyo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigara 'King'  wakifafanua jambo wakati wa shughuli ya   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi
Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigara 'King' akizungumza na wananchi juu ya hatua ambayo serikali imeendelea kufanya katika kushughulikia miundo mbinu mbali mbali ndani ya Nchi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipanda mti kwenye viwanja vya ndege Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita.

Wabunge wa Mkoa wa Geita wakipanda mti wakati wa sherehe za   uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara na mkoa wakikata utepe kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa mkoa wa Geita unaojengwa wilayani humo kwenye sherehe zilizofanyika leo Jumamosi Novemba 4, 2017. Uwanja huo ambao utakuwa na njia yenye urefu wa kilomita 3, unajengwa na makandarasi wazalendo.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ambaye ni Mbunge wa Chato,akitoka kusalimiana na wananchi wa jimbo lake.

No comments:

Post a Comment