Muonekano wa stendi ya mabasi ya Mkoa wa Geita ikiwa imejaa maji kwenye baadhi ya maeneo. |
Wafanyakazi wa Stendi ya Mabasi makubwa Mkoani Geita wamelalamikia ubovu
wa miundo mbinu ya stendi hiyo nakudai kufanya kazi katika mazingira
magumu kwa sababu ya wingi wa maji ndani ya stendi hiyo wakati wa mvua za
masika.
Akizungumza kwaniaba ya wafanyakazi hao Khalid Hassani alisema
matengenezo ya stendi hayakukidhi vigezo ndio sababu inayopelekea
kuharibika mara kwa mara.
“Tumekua tukifanya kazi hapa stend lakini katika mazingira magumu
kwasababu matengenezo ya stendi hayakukidhi haja wala vigezo hata matuta ya
upande wakupaki magari yanayo ingia na kutoka hayapo na tumefikia hatua ya
stendi kua na madibwi mengi kutokana na maandalizi kutokua mazuri’’ alisema
Hassani.
Hassani alisema imekua ni aibu kwao wafanyakazi wa stendi hiyo kwa wageni
wanao ingia na kutoka kutokana na hali ilivyo na Mkoa ambavyo umekuwa ukisifika
kuwa na madini mengi ya dhahabu.
Kwa upande wake mmoja wa wafanya biashara Bi, Anipha Danieli
alisema ndani ya stendi kuna maji mengi hali inayosababisha kujaa kwa
maji kwenye maeneo mengi.
“Mimi tangu tumeanza kuongea leo sio mara yangu ya kwanza tumechoka
kuongea humu mwisho wake tutafuga samaki hii sio stendi jaman hata Geita napo
tunatakiwa tuwe na stendi nzuri na iwe ya kisasa dhahabu zinatoka hapa lakini
stendi yake sio tumeugua fangasi za miguuni kwaajili ya tope zilizomo humu’’
alisema Daniel
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi
Modest Apolinary, alisema watu walitumia vibaya fedha za uma kutokana na
kutokua na uaminifu na ameongeza kuwa wao kama halmashauri wanalitambua tatizo
hilo na ameahidi kumwaga kokoto katika stend hiyo mapema wiki ijayo .
“kwa bahati mbaya hatukuwa na watu waaminifu watu walitumia fedha za uma
vibaya ila uhalisia wa thamani ya fedha haikuonekana mwaka jana
tulitumia zaidi ya milioni ishirini na moja {21} mpaka million ishirini
na tisa{29} kurekebisha na mwaka huu tena tunalijua hilo tumetenga million
ishirini na moja{21} tunategemea kuanzia wiki kesho kufanya marekebisho”
alisema Apolinary.
Apolinary alisema wanampango wa kutangaza tenda kwaajili ya kujenga
stendi mpya Magogo ili kutibu tatizo hilo nasio kumwaga pesa kila siku
kwa ajili ya marekebisho ya kila siku.
No comments:
Post a Comment