Mkuu wa wilaya ya
Chato mkoani Geita Mh. Shabani
Ntarambe amesema hatawavulia wala kuwaonea aibu baadhi
ya wafanyabiashara watakao uza mbolea kinyume na bei elekezi iliyopangwa
na serikali.
Akizungumza na storm
habari wilayani humo mkuu huyo amesema kuwa tayari wameshatoa elimu
kwa viongozi wa vijiji na kata juu ya uuzwaji wa mbolea nakuwataka
wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo na mifugo kuhakikisha wanafuata bei
elekezi iliyo tolewa na serikali ili kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye
tija
Amesema atawachukulia
hatua kali za haraka baadhi ya wafanyabishara wanao haribu ubora wa
mbolea nakuwa uzia wakulima makapi ya mbolea wilayani humo.
Kwa upande wake
Diwani wa Kata ya Buziku Bw.
Magomamoto Zanzibar ameunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya
nakusema kuwa kwa mfanya biashara yoyote katika kata yake atakae bainika
na tuhuma hiyo hata sita kumfikisha mahakamani
No comments:
Post a Comment