Friday 17 November 2017

RC GEITA AAGIZA WAKAGUZI WA NDANI KWENDA MGUSU KUKAGUA MAPATO NA MATUMIZI

DSC_2358

Mhandisi Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita.

DSC_0405
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akishiriki kuchimba msingi wakati wa zoezi la kuhamasisha ujenzi wa zahanati kwenye Mtaa wa Nyakato ambao upo kata ya Buhalahala.

DSC_0427
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akihaidi kuchangia mifuko mia moja kwenye ujenzi wa zahanati ya mtaa wa nyakato.

DSC_0447
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipokea maelezo juu ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Mgusu kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mgusu,Pastory Ruhusa wakati alipotembelea na kushirikiana na wananchi kwenye shughuli za ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.

DSC_2269

Akina mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata za jirani.

DSC_2311

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi  wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya Sekondari.
 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita mhandisiModest Apolinary kupeleka wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha kuhusu mapato na matumizi ya Kata hiyo.

Akizungumza kwenye ziara yake mjini Geita ya kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati Mhandisi Luhumbi amepokea malalamiko ya wakazi wa Machinjioni waliodai kutosomewa taarifa za mapato na matumizi ya fedha zao.

Mhandisi Luhumbi alisema kuwa endapo kama  itakabainika kuwa kiongozi wa mtaa, kijiji au Kata ametumia vibaya fedha za wananchi anapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na kuzirejesha fedha hizo.

“Mkurugenzi leta timu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika".  Alisisitiza Luhumbi.

Mheshimiwa Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 kisha apate taarifa hiyo ofisini.  Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo changamoto nyingi katika maeneo yao.

Diwani wa Kata ya Mgusu Bw Pastory Ruhusa amemueleza Mkuu wa Mkoa changamoto wanazokumbana nazo kutokana na kukosekana kwa kituo cha afya kuwa ni pamoja na wakina mama kujifungulia njiani na muda mwingine watu wengi wamejikuta wakipoteza maisha kutokana na kukosekana kwa zahanati kwenye kata hiyo.

“Mkuu hapa tumezungukwa na mgodi na ulituhaidi kutuchangia sh,milioni mia moj lakini tunaona kama ni maneno tu kwani sasa imepita miaka miwili mgodi haujatekeleza hiyo ahadi kiukweli tunapata shida sana kutokana na kwamba kata yetu ni mpya na uhitaji ni mkubwa sanaa tunaomba msaada wako”Alisema Ruhusa.


Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake ya Mkoa mzima katika Halmashauri ya Mji Geita kwa kutembelea na kushirikiana na wananchi kujenga nyumba pacha ya walimu (Two in one) Shule ya Msingi Shinamwendwa, ujenzi wa kituo cha Zahanati Mtaa wa Nyakato , ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari Mgusu pamoja na kukagua eneo la kujenga Zahanati katika Kata hiyo.  Katika ziara hiyo ya Mkoa mzima Mheshimiwa Gabriel amefanikiwa kutembelea Wilaya zote tano (5) na Halmashauri sita(6) na kufanikiwa kujenga, kutembelea na kuanzisha jumla ya miradi 19 katika Sekta za Afya, Maji na Ujenzi huku akikusanya zaidi ya mifuko 800 ya Saruji, tofali za Block 500, Mbao 50. Haya yote ni matokeo ya kazi aliyoianza ya kushirikiana na wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila kijiji ndani ya Mkoa huu lengo kuu likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na maeneo yao pia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Mkoa humu.

Wananchi wote katika maeneo aliyopita kufanya kazi wameonyesha kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali na kuamua kuunga mkono juhudi hizi kwa kushiriki katika utekelezaji wa miradi kama vile kusoma maji, kubeba mawe, mchanga, kokoto, kuchimba misingi na vijana kujitolea kujenga miradi hii.

No comments:

Post a Comment