Walimu wa wilaya ya Geita wakiwa kwenye Kikao cha kujadili maendeleo na changamoto ndani ya chama cha walimu Wilaya ya Geita. |
Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Geita,John Kifimbi akisoma risala kwa Mgeni rasmi. |
Baadhi ya wageni waalikwa ambao wanatoka taasisi mbali mbali wakifuatilia kikao hicho. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa vyeti kwa walimu ambao wamefanya vizuri ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa chama cha walimu(CWT) Wilaya ya Geita, Alfred Alexander akiwasisitiza walimu kuendelea kuwa na mshikamao ndani ya chama hicho. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza walimu kujingea tabia ya kuwa na vitega uchumi mbali mbali kwenye mazingira ambayo wanafanyia kazi. |
Walimu Wilayani Geita wametakiwa kutumia nafasi walizonazo katika kujiinua kiuchumi kwa kuwekeza kwenye Shughuli za ujasiriamali.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita,wakati wa Mkutano mkuu wa
chama cha Walimu (CWT)Wilaya ya Geita ambao umefanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa halmashauri ya Mji lengo likiwa kuangalini ni kipi
chama kimefanya ndani ya miaka Miwili.
Alisema kuwa wakati umefika kwa walimu kuwekeza katika
fursa za ujasiriamali na kutokuogapa kukopa na kwamba kama kuna mtu ambaye
anampiga vita mwalimu kuwekeza na huku anatekeleza majukumu yake ya msingi ni
sawa na kutokumtendea haki.
“Lengo la kuandaa vitega uchumi
kabla ya uzee na manufaa ya uwekezaji ni kwa manufaa ya jamii kwa hiyo walimu
kama kuna mtu anakupiga vita kwa ajili ya uwekezaji na unafundisha kwa wakati
sahihi mtu huyo nipeni taarifa” Alisema Kapufi.
Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoani Humo,Mwl Lusato Zabron Mashauri
,ameelezea kuwa hali ya kiuchumi bado ni mbaya kwa walimu hususani wale ambao
wanaishi vijijini wengi wao wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kutokana na
viongozi wengi wa kisiasa kutokuwa na uelewa juu ya haki za walimu.
“Hali ya kiuchumi kwa walimu hairidhishi
hususani wale ambao wanaishi vijijini kwani wengi wao wamekuwa wakipigwa vita
na viongozi wa kisiasa mwalimu anapojaribu kuinuka kiuchumi anapigwa vita na
viongozi hao” Alisema Lusato.
Kemilembe Gerigori ambaye anawawakilisha walimu wanawake Mkoani
Humo,alisema hali ya mazingira ya walimu ni magumu kutokana na namna ambavyo
wamebanwa katika suala la muda wa masomo hivyo wengi wao wamekuwa wakishindwa
kujishughulisha na ujasiriamali kwa kukosa muda.
No comments:
Post a Comment