|
Baiskeli ambazo zimetolewa kwa wawakilishi wa kujitolea kwenye jamii na shirika lisilo la kiserikali la plan international mkoani Geita. |
|
Kushoto ni meneja wa Plan Mkoani Geita, Bw Marcel Madubi na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakizungumza wakati wa zoezi la utoaji wa baiskeli. |
|
Meneja wa Plan Mkoani Geita, Bw Marcel Madubi akizungumzia malengo ambayo yamepelekea wao kutoa Baiskeli hizo kwa wawakilishi wa jamii. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wanufaika wa Baiskeli hizo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiendasha Baiskeli ambazo zimekabidhiwa kwa wawakilishi wa jamii. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkabidhi Baiskeli Bi,Lucy John(Katikakati)pembeni kutoka kulia ni Mejena wa Plan ,Bw Marcel Madubi. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkabidhi Baiskeli,Mzee Geofray Kilomba na pembeni ambaye anapiga makofi ni,meneja wa plan Bw,Marcel Madubi.(PICHA NA JOEL MADUKA) | | | |
Shirika lisilo la kiserikali la Plan International ambalo
linashugulikia masuala ya kulinda na kutetea haki za watoto
hususani wa kike limekabidhi Baiskeli kwa wawakilishi wa kujitolea kwa
jamii kwaajiri ya kurahisisha kuwafikia walengwa na kutoa elimu
dhidi ya ulinzi wa mtoto.
Akizungumza wakati wa zoezi la kutoa baiskeli 191 zenye gharama ya
shilingi milioni 39,Meneja wa plan Mkoani Geita,Bw Marcel Madubi alisema kuwa
watoto wangi wamekuwa wakikumbwa na matatizo mengi likiwemo
swala la mimba za utotoni na kuhozwa mapema kitu ambacho kinaweza
kukatisha ndoto zao za kimasomo.
“Wawakilishi wamekua ni kiungo kibwa kati yao na jamii katika
kutafuta takwimu sahihi za watoto na kuwatafutia ufadhili na tangu plan ifike
Geita kume kua na msaada wakuwatoa watoto kwenye utumikishwaji wa kazi zisizo
sahihi mfano kwenye maeneo ya migodi tumeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa” Alisema Madubi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita Herman kapufi ambae alikua
mgeni rasimi katika hafra hiyo alisema msingi wowote wa maendeleo unaanzia na
mtoto kwahiyo ili Taifa liende mbele nilazima watoto waangaliwe kwa
umakini na kwamba chombo ambacho wamepatiwa wawakilishi kitawasaidia kwa kiasi
kikubwa kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Bi,Scholastika Vitus ambaye ni mmoja kati ya wanafaika wa usafiri huo,
alisema kunachangamoto nyingi zinawakumba watoto kama ukosefu wa mabweni hali
ambayo inapelekea wengi wao kujikuta wakiingia kwenye mahusiano na waendesha
boda boda ili mradi waweze kupata usafiri na kwamba endapo serikali itatilia
maanani ujenzi wa mabweni itakuwa imemsaida mtoto wa kike kuepukana na
vishawishi.
No comments:
Post a Comment