Rais
Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe (kushoto) wakifuatilia yaliyokua yakiendelea wakati wa
uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za
kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126
jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi JTV Bw. Sanctus Mtsimbe
Mkurugenzi
Jason’s TV Bw. Sanctus Mtsimbe
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua
ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha
star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bw. Benson Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli
Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bibi. Joyce Hagu
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua
ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha
star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli
Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli
Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akibonyeza rimoti kuzindua Chaneli
ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe
Rais
Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete(waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya filamu baada ya
kuzindua Chaneli ya Jason’s TV (JTV)
itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika
king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam. Wanne
kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
Rai hiyo imetolewa
na Rais Mstaafu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alipokua akizindua chaneli mpya ya Jason’s Televisheni itakayokuwa ikionyesha
filamu mpya za kitanzania inayopatikanakatika king’amuzi cha Star times chaneli
namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
“Wadau wa tasnia ya
filamu nchini hasa waandaaji wa filamu mnapaswa kuangalia namna ya kupata wadau
watakaosaidia kuwekeza vifaa vya kisasa vya kurekodia na kwa upande wangu
nitajaribu kuwakutanisha na wadau wenye uwezo wa kuwekeza ili muangalie namna
ya kuzungumza nao na kuwekeza vifaa vitakavyowawezesha kuandaa filamu zenye
ubora na kukidhi hadhi ya kushindana kimataifa” amesema Mhe. Kikwete.
Aidha Mhe. Kikwete
amesema kuwa kuwepo kwa chaneli ya JTV itakayokua ikirusha filamu mpya za
kitanzania ni jambo muhimu sana katika historia ya tasnia ya filamu hapa nchini
hivyo uzinduzi wa chaneli ya JTV unafungua ukurasa mpya katika maendeleo ya
tasnia ya filamu ambayo imekua ikikua kwa kasi.
Mhe. Kikwete amesema
kuwa kufanikiwa kwa chaneli ya JTV
kutapunguza machungu mengi ya watayarishaji wa filamu kwa kutatua
changamoto ya kutokuwa na soko la uhakika na kuleta nuru ya matumaini kwa
wasanii kwa kupata malipo yanayostahili
kwa vipaji vyao, jasho lao pamoja na gharama wanayoingia katika kutengeneza
filamu.
Kwa upande wake
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amesema kuwa uanzishwaji wa chaneli ya JTV ni moja ya mikakati kadhaa ya
kuboresha usambazaji wenye tija wa filamu mpya za kitanzania hivyo kuwataka
watayarishaji wa filamu kuthamini mandhari za filamu zetu kwani filamu
iliyokosa hata dakika moja kuonyesha vivutio vya utalii tulivyonavyo inakosa
sifa ya ubora.
Awali Mhe. Mwakyembe
amesema kuwa Tanzania itabaki kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ambayo ni
lugha ya 10 kuzungumzwa na watu wengi duniani kati ya lugha 6000 hivyo ni
matarajio ya wizara baada ya muda mfupi mtu akisikia ala za nyimbo za Kiswahili
katika filamu zetu kama vile Mdumange, Sindimba nk. ajue anaangalia filamu ya
kitanzania.
Naye Kaimu Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bw. Benson Mkenda
amesema kuwa bodi ya filamu ipo tayari kushirikiana na wadau wote katika tasnia
ya filamu wenye nia ya kukuza na kuendeleza tasnia kama ilivyo kwa Jason’s TV
ambao lengo lao mahususi limelenga kuendeleza sekta ya filamu hasa katika eneo
la usambazaji ili kuweza kuitoa sekta hii mahali ilipo na kuifikisha katika
viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment