Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo
Baadhi ya wananchi wilayani Chato mkoani
Geita wameahidi kushirikiana na mkuu wa mkoa Mhandisi
Robart Gabriel kwa kuwa ameonesha dhamira ya kuleta mabadiliko mkoani
hapa.
Kauli hiyo
wameitoa wakati wakifanya usafi katika eneo linalo tarajiwa kujengwa kituo cha
afya cha kata ya mganza ambapo wamesema kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza
vifo vya akina mama wajawazito na watoto
Kwa upande
wake mganga mkuu wilayani humo Dakta Atanas Ngambakubi amebainisha
kuwa wataanza na ujenzi wa jengo la huduma ya wagonjwa kisha kufatia nyumba za
watumishi kwa lengo la kukifanya kituo hicho kuwa kinatoa huduma wakati wote.
Nae mkuu wa
wilaya ya chato Bw Shaban Ntarambe amesema kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka
huu zoezi hilo litakuwa limekamilika.
No comments:
Post a Comment