Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu inatarajia kuanza kusikiliza ushahidi wa kesi ya kumtolea lugha ya
matusi Rais John Magufuli inayomkabili mbunge wa Kawe, Halima Mdee (39),
December 7, 2017.
Wakili wa serikali,
Leornad Challo amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa kesi imeitishwa
kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini shahidi waliyenaye ana safari.
Baada ya kuelezwa
hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi December 7, 2017 kwa ajili ya
kuanza kusikilizwa.
Awali katika kesi hiyo
Mdee aliposomewa maelezo ya awali inadaiwa July 3/2017 akiwa Makao Makuu ya
Chadema, maeneo ya Ufipa alitoa lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli.
Inadaiwa alitukana
kuwa “Rais anaongea hovyo hovyo, inabidi afungwe break”.
Baada ya kutoa lugha
hiyo, July 4/2017 alikamatwa na Polisi maeneo ya Kibangu, kisha kupelekwa kwa
ZCO ambapo alihojiwa na kukiri kutoa maneno hayo.
Baada ya kusomewa
maelezo hayo, Mdee alikubali wasifu wake ambao ni Jina, umri, nafasi ya
uongozi, mahali anapokaa, kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Lakini alikana
kumtolea lugha ya matusi Rais Magufuli, pamoja kukiri maneno hayo wakati
akihojiwa katika ofisi za ZCO.
No comments:
Post a Comment