Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufu akishiriki zoezi la ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kasota. |
Wananchi wakishiriki zoezi zima la ujenzi wa zahanati. |
Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita Dkt Raphael Mhina akishiri zoezi la ujenzi wa zahanati kwenye kijiji na kata ya Kasota. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki ujenzi wa madarasa shule ya msingi Ludete(Picha na Joel Maduka) |
Mkuu wa mkoa wa Geita
Mhandisi Robert Luhumbi ameendelea na za ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja
na zahanati kwenye kata za Ludete na Kasota lengo likiwa kupunguza changamoto
za kimiundombinu zinazoukabili Mkoa huo ambao ameutaja kuwa wa mwisho katika suala
hilo
Akizungumza na
wakazi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita , Mhandisi Luhumbi alisema wananchi
wana moyo wa kujitoa na kutaka maendeleo lakini wanakwamishwa na ukubwa wa
gharama za wakandarasi kwenye baadhi ya miradi
“taarifa nilizozipata
ni mbaya katika mkoa wetu mkoa huu niwa mwisho katika mambo ya miundo mbinu
takwimu hizi ziliniamsha nisikae ofisini nina mikakati ya kuhakikisha
zahanati zinajengwa kwa kila kijiji ,mitaa na hata kata ’’Alisema Luhumbi
Luhumbi alisema
baadhi ya watendaji wamekuwa wakitumia miradi ya maendeleo kujinufaisha na
kutaka bei elekezi ya gharama za ujenzi itolewe ili wananchi wajenge miradi yao
na fedha ziwanufaishe wananchi husika
“nimegundua wananchi
wanamoyo wa kujitolea lakini waanaangushwa na wakandalasi gharama nikubwa mno
ambayo wanakutana nayo alafu miradi haikamiliki kuanzia wakati huu tutatoa bei
elekezi na mkandalasi ni marufuku kwa Mkoa wa Geita kwa majengo ya shule
madarasa watajenga wananchi husika’’
Mhandisi Luhumbi
amewapongeza wananchi kwa jitihada zao na kwamba bado Serikali inahitaji juhudi
zao huku akiwahakikishia kuwa ofisi yake itashirikiana nao ili kuondoka kwenye
nafasi ya mwisho katika masuala ya Kimiundombinu
No comments:
Post a Comment