|
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akipatiwa maelezo na mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George wakati walipokuwa wakitembelea maktaba ya jamii ambayo hipo wilayaniNyang’hwale ,katika kati ni katibu tawala wa Wilaya hiyo Fabian Sospeter. |
|
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akikata utepe na katibu tawala wa Wilaya yaNyang’hwale Bw,Fabian Sospeter wakati wa zoezi la kukabidhi maktaba hiyo. |
|
Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo. |
|
Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo. |
|
|
Meneja Ufanisi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,Bw Elias Kasititila akielezea namna ambavyo wameguswa kuchangia maktaba hiyo. |
|
Bi,Vannesa Kasoga akisoma taarifa ya ukamilikaji wa maktaba hiyo tangu ilipoanza kufanyiwa maboresho na kampuni ya ACACIA. |
|
Mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George akielezea namna ambavyo wameweza kufanukisha kuhakikisha maktaba inakuwa kwenye muonekano bora. |
|
Katibu tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter akiwasisitiza wananchi pamoja na wanafunzi kutumia maktaba hiyo kujifunza mambo mbali mbali. |
|
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi na kuzindua maktaba ya jamii wilayani Nyang’hwale. |
|
Wananchi ambao wamejitokeza kwenye zoezi la uzinduzi wa Maktaba. |
|
Wanafunzi wa shule ya Msingi Karumwa wakiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya jamii. |
Mgodi wa acacia Bulyanhulu kwa kushirikiana na shirika lisilo la
kiserikali la read international wamekabidhi maktaba ya kisasa ya
jamii ambayo imetumia kiasi cha sh,milioni 23 hadi kukamilika
kwake kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale ambayo itawasaidia
wananchi kupata maarifa na kujifunza mambo mbali mbali kutokana na vitabu
ambavyo vinapatikana.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi wa maktaba ya
jamii,meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu alisema kuwa
wanaamini katika kufikia Tanzania ya viwanda basi ni vyema watu wakawa na
ufahamu ambao utawasaidia kujua fursa mbali mbali ambazo zinawazunguka hivyo
kupitia maktaba hiyo wananchi wanaweza kusoma vitabu ambavyo vitawasaidia kujua
mambo mbali mbali.
“Tunatambua umuhimu wa elimu na tunaimani kuwa
jamii ya Wilayah ii itatumia vyema Maktaba hii kwa kusoma na pia kujifunza
mambo mbali mbali ambayo yamo kwenye vitabu ambavyo vipo kwenye maktaba hii
hivyo tunaomba iweze kutunza kama vile sisi tulivyoikabidhi ikiwa katika hali
nzuri” Alisema Busunzu.
Hata hivyo kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya Hiyo Fabian
Sospeter aliwataka wananchi pamoja na wanafunzi kujenga desturi
ya kupenda kusoma vitabu mara kwa mara na kwamba kufanya hivyo
wataweza kujua mambo mengi zaidi.
“Wananchi niwasisitize kutumia maktaba hii kujifunza na kusoma masuala
mbali mbali na ndani ya maktaba hii kuna vitabu vya kilimo ambavyo vitawasaidia
wakulima kulima kilimo cha kisasa na ambacho kitawaletea faida”Alisema Fabian
Bw Mabura Makonga na Georgi John walisema kuwa wanaamini kuwa maktaba
hiyo itawasaidia kujua mambo mbali mbali huku wakishauri elimu itolewa zaidi
kwa wananchi kutambua umuhimu wa kujenga tabia ya kupenda kujisomea
kwani wengi wao awana elimu na jambo hilo ni geni kwenye Wilaya hiyo.
Hata hivyo Bi,Vannesa Kasoga ameelezea uhaba ambao wanao kwenye maktaba
hiyo kuwa ni upungufu wa kompyuta saba,mashine ya kuzalisha nakala
na upungufu wa baadhi ya vitabu.
No comments:
Post a Comment