Sunday 5 November 2017

GGM YAENDELEA KUFADHILI MATIBABU KWA WATOTO WENYE MIDOMO SUNGURA

Mtoto ambaye anatatizo la mdomo sungura akisubilia kwenda kufanyiwa matibabu Jijini Mwanza wakati wa hafla ya kuwaaga.

Mratibu wa kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi akisisitiza jamii kutokuwa na dhana ya kuwatenga na kuwanyanyapaa watoto ambao wanakuwa na matatizo ya midomo sungura.

Meneja  mahusiano kwa jamii wa Mgodi wa GGM Bw.Manase Ndoroma  akielezea namna ambavyo wameendelea kuendesha zoezi la kutoa msaada wa matibabu kwa watoto wenye tatizo la mdomo sungura tangu mwaka 2004.

Mkurugenzi mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson,akielezea juu ya gharama ambazo wametumia hadi sasa tangu walipoanza mpango wa matibabu kwa watoto ambao wanamidomo sungura.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwapa maneno ya faraja wakati alipokuwa akiwaaga watoto pamoja na wazazi ambao wanatarajia kwenda mwanza kwaajili ya matibabu.

Mkurugenzi mkuu wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson na  Mratibu wa kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi wakimsikiliza mkuu wa Wilaya.

Watoto wenye tatizo la midomo sungura wakiwa na mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mkuu wa mgodi wa GGM kwenye picha ya pamoja.
                                                   Mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi amewataka wazazi na walezi wenye  watoto ambao wanamatatizo ya midomo Sungura,Mtindio wa ubongo na ulemavu mwingine kutowanyanyapaa watoto wao badala yake kuwatolea taarifa kwa wataalamu wa afya ili serikali iwatambue nakuwatafutia matibabu.


 Hayo aliyasema wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watu wenye matatizo ya midomo Sungura wanaosafiri kwenda jijini Mwanza kupatiwa Matibabu ambayo yanadhaminiwa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM).

 Mkuu wa wilaya alisema matibabu ya watu hao yanafadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Geita GGM kwakushirikiana na Shirika moja la Australia liitwalo Rafiki Mission hivyo ni vyema kwa jamii pindi wanaposikia matangazo kujitokeza kwa kuwapeleka watoto wao au ndugu zao kujiandikisha kwaajili ya kupatiwa matibabu.

Akitoa taarifa ya Mkurugenzi wa Mgodi wa GGM Richard Jordinson kuhusu matibabu ya watu hao, Meneja  mahusiano kwa jamii wa Mgodi wa GGM Bw.Manase Ndoroma alisema tangu kuanzishwa kwa Mpango huo wa   matibabu kwa watu wenye midomo ya sungura mwaka 2004, Mgodi wa GGM umetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1 hadi sasa.

Bi.Mwajuma Morris, ni mmoja wa wazazi wenye watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo Sungura ambao ni miongozi mwa watoto wanaosafirishwa kwenda Hospitali ya Seketule Jijini Mwanza kwaajili ya matibabu ameelezea kuwa mtoto wake amekuwa akitengwa na jamii na muda mwingine watoto wenzake wamekuwa wakimcheka anapokuwa shuleni hali ambayo inamfanya kujiona ananyanyapaliwa na jamii ambayo inamzunguka.

Kwa upande wake mratibu wa kitengo cha afya Mgodini GGM Dkt.Kiva Mvungi aliwataka wananchi kujiepusha na vitendo vya unyanyapaa kwakuwa tatizo hilo sio laana.




No comments:

Post a Comment