Thursday, 2 November 2017

HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUFANYA MANUNUZI BILA WAKANDARASI


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege (mwenye suti ya kaki) akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo Jimbo la Itilima Njalu Silanga (mwenye shati jeupe) wakikagua miradi ya maendeleo jimboni humo.


Wananchi wa Kijiji cha Senani wakimshuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege alipokuwa akiweka jiwe la Msingi katika zahanati ya kijiji hicho.



Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege (mwenye suti ya kaki) akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo la Itilima Njalu Silanga wakikagua na kuona ujenzi wa jengo la halmashauri ya Itilima.


Ujenzi wa Tanki la Maji katika kijiji cha Ikungulipu wilayani Itilima, alipokuagua Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege jana.


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Kandege akiongea na wakazi wa kijiji cha Migato (hawapo pichani) juu ya ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya  
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege amezitaka Halmashauri zote nchini kufanya manunuzi ya bidhaa bila kutumia wakandarasi (force account) ili kupunguza gharama za ujenzi wa miradi.

Kandege aliyasema hayo jana wakati akikagua, kuona na kuweka mawe ya msingi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, zahanati na mradi wa maji wilayani Itilima mkoani simiyu.

Alisema kuwa serikali ingependa Halmashauri zitumie force accont ili kupunguza gharama za ujenzi wa miradi kwa sababu wakandarasi wengi wamekuwa wakipandisha bei ya bidhaa kuliko uhalisia.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa Nyumba nne za watumishi, Afisa Mipango wilaya ya Itilima Paulo Nyalaja alisema kuwa nyumba hizo za zitapunguza suala la uhaba uliokuwa unawakabili watumishi hao.

Alisema kuwa nyumba hizo zinajengwa na mkandarasi wa kampuni ya Gati Eng. Co. Ltd ambapo zimegharimu milioni 268 huku kila nyumba ikijengwa kwa milioni 67.

Mbunge wa Jimbo la itilima Njalu Silanga alisema kuwa katika Jimbo hilo kuna Majengo 28 ya zahanati yaliyofikia hatua ya ukamilishaji kwa nguvu za wananchi na kuitaka serikali kuunga mkono juhudi za wananchi.

Aliongeza kuwa shule ya msingi Migato ina uhaba wa vyumba vya madarasa wakati huo ikiwa na wanafunzi 1933, na kumtaka Naibu waziri kuzipa kipaumbele cha usajili shule shikizi na shule bubu.

Naibu Waziri Kandege aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Nyumba za watumishi Itilima, zahanati Senani, madarasa ya manne ya shule ya msingi migato, kukagua ujenzi wa jengo la halmashauri, mradi wa maji Itilima Ikungulipu.

No comments:

Post a Comment