Wananchi wa Kata ya Buhalahala Mtaa wa Mwatulole wakiwa kwenye zoezi la kusajiliwa kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa. |
Baadhi ya watumishi wakiwa kwenye zoezi la uandikishaji wananchi vitambulisho vya Taifa. |
Mratibu wa NIDA Mkoani Geita,Bw Emmanuel Ernest akitoa elimu kwa wananchi juu ya zoezi la uandikishaji. |
Wakazi laki moja na elfu kumi na mbili(112000)katika Halmashauri ya mji wa Geita wameandikishwa kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya taifa .
Zoezi la kuandikisha wananchi kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa
limeanza mwezi August Mwaka huu na kwamba kwa mujibu wa sense ya mwaka 2012 ni
watu Laki moja na elfu themanini na saba wanatarajia kuandikishwa kwenye
halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Apolinary
aliesema zoezi hilo limekuwa na mwitikio mzuri na wengi wanatamani kupata
vitambulisho hivyo.
“Pamoja na changamoto ambazo zimejitoeza kwa
baadhi ya wananchi lakini tunashukuru limekuwa na mwitikio mkubwa sana kwani
watu wengi wamejitokeza kuandikishwa” Alisema Apolinary.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alieleza kuwa wamelenga
kufikia mwezi Oktoba mwakani wawe wameandikisha wananchi wote kwenye
halmashauri ya mji na ya Wilaya kufikia watu elfu tano.
Bw Joseph Bwire ambaye ni mkazi wa Mtaa wa mkoani na Bi Magdalena
Manyirizu walisema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutambulika na
pia kupata mikopo kwenye mashirika ya kifedha.
Afisa usajili wa NIDA Mkoa wa Geita Bw Emmanuel Ernest alisema
wanatarajia kwenye Mkoa mzima kusajili wananchi milioni moja wenye sifa ndani
ya Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment