Baadhi ya wadau wa sekta ya madini Nchini na wachimbaji wadogo wakiwa kwenye mjadala ambao umeandaliwa na Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na maendeleo(IIED )wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali hakimadini,Kampuni ya ushauri(MTL) na kituo cha kimataifa cha utafiti wa mistu(CIFOR) na kufanyika kwenye ukumbi wa hotel ya alphendo Mkoani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha mgeni Rasmi kwaajili ya kuzungumza na wadau wa sekta ya madini wakati wa Mkutano wa majadiliano juu ya swala la uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo.
Kamishina msaidizi wa madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo ambaye pia ni mgeni rasimi , Mhandisi David Mulabwa akifungua majadiliano hayo mapema hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa alphendo hotel.
Bw. Fitsum Weldegiorgis kutoka Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na maendeleo(IIED ) akielezea namna ambavyo taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli pamoja na sekta ya madini Nchini.
Rebecca Burton ambaye anatoka taasisi ya Tiffany akizungumza namba ambavyo taasisi yao inafanya kazi wakati wa Mkutano wa majadiliano.
Mtafiti wa kampuni ya ushauri Dkt,Willson Mtagwaba,akibainisha changamoto ambazo wamekutana nazo wakati wakifanya tafiti kwa wachimbaji wadogo.
Baadhi ya wadau wa sekta ya madini wakiwa kwenye makundi kwaajili ya kujadili mambo kadha wa kadha.
Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na maendeleo(IIED )wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali hakimadini,Kampuni ya ushauri(MTL) na kituo cha kimataifa cha utafiti wa mistu(CIFOR) imewakutanisha wachimbaji wadogo wa madini lengo likiwa ni kutazama na kuona sekta ya madini inavyowahusisha wachimbaji wadogo kwenye shughuli za uchimbaji Mkoani Geita.
Kamishina msaidizi wa madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo ambaye
pia ni mgeni rasimi , Mhandisi David Mulabwa akifungua majadiliano hayo mapema
hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa alphendo hotel,alisema kuwa
tatizo ambalo linawakabili wachimbaji wengi ni kutokuwa na mitaji ya kutosha
kwaajili ya kufanya shughuli za uchimbaji kwenye maeneo ambayo yanakuwa na
wingi wa madini (MASHAPU).
“Sasa ili kupata wingi wa madini ambayo yapo
kwenye Mashapu kunaitajika nguvu kubwa ya mitaji sasa wachimbaji wetu wengi
awana mitaji ya kutosha na ndio maana unakuta watu wanachimba tu bila ya kuwa
na taarifa za mashapu sasa unapokuwa una taarifa za mashapu ujui unatumia
shilingi ngapi na utapata shilingi ngapi kwa hiyo inakuwa shughuli
ya kubahatisha sasa ili uchimbaji uwe wa tija tunawaelimisha ni vizuri wakawa
wanatafuta namna ya kupata taarifa za mashapu kwenye maeneo yao” Alisema Mulabwa.
Kwa upande wake Mtafiti wa kampuni ya
ushauri Dkt,Willson Mtagwaba alibainisha kuwa wakati wa shughuli za
kuwazungukia wachimbaji wadogo wamebaini tatizo kubwa wengi wao wamekuwa sio
rasmi hali ambayo imeendelea kuleta migogoro baina ya wao na wachimbaji wakubwa
na jambo jingine ni kutokuwepo kwa mikopo na bei elekezi.
Bi,Mathar Bitwa ambaye ni mchambaji wa madini ameeleza kuwa bado wanawake
wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya madini kutokana na kutokupewa
kipaumbele kwenye shughuli hizo na kuwepo kwa mila na desturi kwa baadhi ya
makabila pamoja na mfumo dume kwenye shughuli hizo za uchimbaji
,huku Bw, Mtalingi Hamza Mohamedi akielezea sababu ambazo zinasababisha
kutokupewa mikopo na mabenki ni kutokana na wao kutokujua kile ambacho
wanakichimba wakati wa shughuli hizo.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya hakimadini,Bw Amani Muhina alisema kuwa
uchimbaji mdogo unatoa fursa sawa kwa watu kubadilisha maisha yao
bila kuwa na ubaguzi wa kipato au Elimu kwasababu uchumi wa nchi unaletwa na
watanzania wenyewe.
No comments:
Post a Comment