Serikali wilayani
Chato mkoani Geita imeahidi kuvitaifisha vyombo vyote vya moto
vitakavyokamatwa vikisafirisha samaki wachanga kutoka ziwa victoria
kwenda maeneo mengine ndani na nje ya wilaya hiyo.
Kauli hiyo imetolewa
na mkuu wa wilaya ya Chato Shabani
Ntarambe wakati akizungumza na storm habari ofisini kwake juu
ya uvuvi haramu mbapo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanakagua magari na
pikipiki kwa lengo la kuwabaini baadhi ya watu wanaosafirisha samaki wachanga
kinyume na sheria.
Amesema hatua hiyo
imekuja mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa
madereva bodaboda na magari ya abiria wanaotumia vyombo hivyo
kutorosha samaki wachanga jambo ambalo halikubariki.
Aidha mwenyekiti wa
uhifadhi wa rasilimali za uvuvi BMU wilayani humo Bw Bashiri Manampa amesema kuwa amejipanga kuanzisha msako mkali kwa kushirikiana
na maofisa wa uvuvi wilayani humo kwa lengo la kuendelea kupambana na wavuvi
haramu katika ziwa victoria.
No comments:
Post a Comment