Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
Akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Leah Komanya Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto , Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt.
Hamis Kigwangala amesema kuwa Serikali inakamilisha maandalizi ya kuanzisha
matibabu ya Saratani kwa kutumia mionzi katika Hosipitali ya Bugando Jijini
Mwanza.
Baadhi ya majengo kwa
ajili ya huduma husika yamekamilika yakiwemo jengo ambalo ni maalumu kwa ajili
ya kudhibiti mionzi ambapo ukuta wake umejengwa kwa zege nene la mita
moja,jengo la kutolea huduma za mionzi, baadhi ya wataalamu wapo na baadhi ya
mashine za matibabu kwa mionzi zimeshanunuliwa zikiwemo Cobalt 60 na CT
Simulator.
“Takwimu zinaonyesha
kuwa katika kipindi cha mwaka 2009-2017 Hosipitali imetoa matibabu kwa wagonjwa
39,300 kati yao 12,200 wakiwa ni wapya sawa na wastani wa wagonjwa wapya 1500
kwa mwaka” Alisisitiza Dkt. Kigwangala.
Akifafanua Mhe.
Kigwangala amesema vifaa vingine ikiwemo brachytherapy na immobilization
devices zinatarajiwa kuwasili mwezi Disemba mwaka huu.
Aidha, kwa sasa huduma
za Tiba ya Saratani zinazopatikana katika Hosipitali ya Bugando ni zile za
matibabu yasiyo ya mionzi (chemotherapy) ambazo zilianza januari 2009 kufuatia
Sera ya Serikali kutoa huduma hizo Kikanda.
Kutokana na msongamano
wa Wagonjwa wanaosumbuliwa na Ugonjwa wa Saratani uliopo katika Hospitali ya
Ocean Road pamoja na gharama kwa ndugu wa wagonjwa, Serikali imeadhamiria
kuboresha huduma za Afya kwa kupanua huduma hizo hadi ngazi ya Kanda.
No comments:
Post a Comment