Tuesday 14 November 2017

WANANCHI WA MGUSU WASHIRIKIANA NA DIWANI KUJENGA SHULE YA SEKONDARI.

Baadhi ya wananchi wa kijiji na kata ya Mgusu wakishiriki ujenzi wa shule ya Sekondari ya kata lengo likiwa ni kupunguza adha ambazo wameendelea kukutana nazo wanafunzi kwa kutembea umbali mrefu kufuata Elimu.

Diwani wa Kata ya Mgusu,akionesha moja kati maeneo ambayo shule hiyo inatarajia kujengwa.

Vifaa vya ujenzi yakiwemo Mawe na Kokote vikiwa kwenye eneo la ujenzi wa shule ya sekondari.

Diwani wa Kata ya Mgusu,Pastory Ruhusa akiwa kwenye eneo la ujenzi na akizungumzia hatua ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ya kata.
Na,Joel Maduka ,Geita.

Wakazi wa Kata ya Mgusu wilayani Geita wameanza kujenga msingi wa shule ya sekondari ya kata hiyo ili kupunguza tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo.

Diwani wa kata hiyo Bw Pastory Ruhusa alisema wananchi wamechangia ujenzi huo ili kuwanusuru wanafunzi wanaolazimika kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

“Wanafunzi wa kata hii wanapata shida sana wanatembea umbali wa kilomita 20 kufuata masomo na muda mwingine kutoka hapa kwenda shule ya sekondari ya shantamaini ni mbali sanaa na usafiri ni washida ndio maana tumeonelea mimi nikiwa kama diwani na wananchi wa kata hii ya Mgusu tuchangishane ili tuweze kujenga shule ambayo tunafikiria kama Mungu itampendeza mwakani waanze kusomea hapa wale ambao wamemaliza mtihani wa shule ya msingi mwaka huu”Alisema Diwani

Baadhi ya wazazi Bi Naomi Barubaru na Bw Mussa Ngozi walisema  tatizo la umbali na kukosekana usafiri maalum wa wanafunzi limesababisha waanze ujenzi huo.

“Ndugu mwandishi kiukweli inatuumiza sana sisi kama wazazi kuendelea kuona watoto wetu wanashindwa kutumiza ndoto zao kutokana tu na umbali wa kufuata masomo tumeonelea ni bora tuanze ujenzi maana hapa tunamgodi wa GGM lakini hauna manufaa yoyote kwenye kata pamoja na kwamba wanafanya shughuli za uzalishaji dhahabu tunasikia tu wanatoa misaada Arusha lakini maeneo ambayo wanapatia hizo mali wananchi tupo hoii”Alisema Mzee Ngozi.

“Mabinti zetu wamekuwa wakikutana na shida sana pindi wanapokwenda shuleni wengine wameshindwa kumaliza kutokana na kupata mimba kwasababu tu ya umbali tunadhani kukamilika kwa shule hii itasaidia wanafunzi kusoma karibu na makazi yao”Alisema Bi,Naomi.

Meneja mwandamizi wa masuala ya jamii kwenye Mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM Bw Manase Ndoroma alisema mgodi huo umetenga fedha za kujenga jingo la utawala kwenye shule hiyo kwa mwaka 2018 baada ya mwaka jana kuwapa wananchi hao Sh Milioni 15.

Wanafunzi hao wanalazimika kutembea umbali wa Kilomita 25 Mgusu kwenda shule ya sekondari ya Mtakuja kufuata masomo .





No comments:

Post a Comment