Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi. |
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga. |
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji. |
Akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa
Halmashauri ya mji wa Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu wa Mkoa wa
Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika
kwenye maeneo ya kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna
pamba nyingi.
“Wito wangu kwa wakulima wote pamoja na
wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba
Mkoani kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia wakulima
kufuata zile kanuni kumi bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia
wakulima lakini nataka twende kisayansi zaidi” Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kumsaidia mkulima na kuwataka wakulima kuchangamkia
fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo cha pamba kwa kuwa hali ya hewa
ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema
lengo ni kuhakikisha wanaongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250
hadi 300 na kwenda kwa wastani wa kilo 800.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta
67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba lakini
utekelezaji ulikuwa hekta 24 791 zilizozalisha tani 13
267.8 zenye thamani ya Sh Bilioni 15.
No comments:
Post a Comment