Thursday, 9 November 2017

MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI BUNGENI LEO MJINI DODOMA


Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akimsikiliza Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni  Mhe.Freeman Mbowe wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Bungeni  Mjini Dodoma. 


Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo  kwa Waziri Mkuu wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiteta jambo na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.



Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Dk Imaculate Semesi  wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.



Mbunge wa Bukombe(CCM) Mhe.Doto Biteko akiuliza swali wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.



Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.



Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.


Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya sekondari Dodoma wakiwa bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za bunge ilo wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza mkutano wa tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Joyce Ndalichako akiwasilisha kauli ya Serikali kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018 Bungeni mjini Dodoma.


No comments:

Post a Comment