Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameishukuru serikali ya watu wa
China kwa msaada wao walioutoa kwa wananchi wa Tanzania wa kuwapatia matibabu
bure, akisema jambo hilo ni upedo usio elezeka.
Rais Magufuli ametoa
kauli hiyo leo alipoenda kutembelea meli yenye madaktari bingwa kutoka China
ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma za vipimo
na matibabu kwa wakazi wa Dar es salaam bila gharama yoyote.
"Tunapenda kusema
shukrani kwa dhati kwa serikali ya China kuamua kuituma meli na madaktari kuja
Tanzania, tunafurahi kwa huduma zao, wameokoa maisha ya watanzania zaidi ya
elfu 6,400, huu ni upendo wa pekee unaogusa, ndio maana leo nimeshindwa
kuvumilia nimeona bora nije nishukuru, nimeguswa mno na ndugu zetu wachina,
yapo mataifa mengine matajiri, yenye mali nyingi lakini hayajaguswa",
amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hayo Rais
Magufuli amewakabidhi madaktari hao barua maalum kwenda kwa raisi wa nchi yao
Xi Jinping pamoja na kinyago kama zawadi kwake, kumshukuru kwa mchango wake na
ukarimu wake kwa watanzania masikini.
Pia Rasi Magufuli
amewatakia safari njema madaktari hao na kuwaomba kurudi tena wakati mwengine,
na kuwataka kukaa kwa muda mrefu zaidi ili waweze kutoa huduma kwa watanzania
wengi hata watakaotoka mikoani
No comments:
Post a Comment