Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akiongozana na kiongozi Mkuu wa Gwaride pamoja na Mshauri wa majeshi ya akiba Wilayani humo,Luteni Kanali ,Daud Issah Mnyanga wakati walipokuwa wakikagua gwaride.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani ,Humo akiimba wimbo wa Taifa mala baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
Baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa zoezi la kufunga mafunzo ya jeshi la akiba(Mgambo).
Baadhi ya askari wa jeshi la akiba wakijiandaa kupita mbele ya mgeni rasmi kwaajili ya kutoa heshima.
Moja kati ya viongozi wa Gwaride akiongoza askari wa Mgambo wakati walipokuwa wakitoa heshima kwa mwendo wa taratibu mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita akitazama shughuli na burudani ambazo zilikuwa zikifanyika wakati wa zoezi hilo.
Gwaride likipata kwa mwendo wa taratibu mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati Gweride lilipokuwa likipita mbele kwaajili ya kutoa heshima.
Makomandoo wa jeshi la akiba wakionesha namna ambavyo wamehiva kwenye suala la kupamba na adui.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ambayo yalikuwa yanafanywa na jeshi la akiba.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwk Herman Kapufi akiwatunuku vyeti baadhi ya askari wa mgambo ambao wamehitimu mafunzo.
Mshauri wa jeshi la akiba wilayani Geita Luteni Kanali ,Daud Issah Mnyanga akimkaribisha mgeni rasmi wakati wa shughuli za kuwaaga askari wa jeshi la akiba.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwahutubia baadhi ya askari ambao wamefudhu mafunzo hayo.
Vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba ama Mgambo wilaya Geita,
wameiomba serikali kuwapa kipaumbele katika fursa za ajira za ulinzi
zinazojitokeza na pia mikataba ya walinzi izingatie maslahi yao.
Akisoma Risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl
Herman Kapufi, Muhitimu wa mafunzo hayo Helena Nyamtondo alisema ni vyema kwa
serikali ikatoa fursa za ajira kwenye Nyanja mbalimbali kwa wahitimu wa mafunzo
hayo yakiwemo makampuni binafsi ya ulinzi ambayo yapo wilayani humo.
“Ndugu Mgeni rasmi tunaomba kupitia mafunzo haya sisi kama wahitimu
tupate nafasi kwenye makampuni ya ulinzi yakiwemo ya G4S na Mgodini kwakuwa
tunaweza kutumia kile ambacho tumefundishwa kuweka usalama kwenye maeneo hayo
na swala jingine ni mishahara na mikataba ya walinzi kutokuwa na masirahi hivyo
tunaomba kuboreshewa masirahi ya kazi zetu” Alisema Bi,Nyamtondo.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi alisema katika
kuhakikisha kuwa anashughulikia maombi yao wiki ijayo atakutana na viongozi wa
makampuni ya ulinzi kuzungumza nao kuona namna wanavyoweza kuwasaidia wahitimu
wa mafunzo hayo kupata ajira kwenye mashirika yao.
Kwa upande wake mshauri wa Mgambo wilayani Geita Luteni Kanali Daud
Mnyanga alisemaa katika mafunzo ya mwaka huu wamekutana na changamoto ya vijana
kutofika kwa wakati na tatizo la kifedha .
Jumla ya wahitimu 195 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo huku
28 wakishindwa kuhitimu kati ya washiriki 223 walioanza mafunzo hayo awali.
No comments:
Post a Comment