Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kufanya
ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 23 - 25
Novemba, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa jana tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina
Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili mjini Songea siku ya Alhamisi
tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika
Uwanja wa ndege Songea majira ya 7.00 mchana.
Baada ya kuwasili
atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama Tawala Uwanja wa Ndege
Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo atafungua ghala la MIVARF,
kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na baadaye ataongea na wananchi wa
Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara.
Ijumaa tarehe 24
Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake kwa kuongea na
wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya ya Tunduru ambapo
atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde na Matemanga akiwa njiani
kuelekea mjini Tunduru.
Aidha, Mheshimiwa
Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala la kuhifadhia
Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika TAMCU. Jioni Mheshimiwa
Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini
Tunduru katika uwanja wa michezo. Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa
Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa Mndeme
ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika
mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea atakapowasili Aidha amewaomba wananchi
kujitokeza kwenye maeneo yote ambayo Waziri Mkuu atapita na kwenye mikutano ya
hadhara ili wapate fursa nzuri ya kumsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea
maelekezo atakayoyatoa.
No comments:
Post a Comment