Wakati zoezi la
umwagiliaji wa dawa za kuua mbu maarufu kama dawa za ukoko likiendelea mkoani Geita
zoezi hilo limekubwa na changamoto kubwa kutokana na wananchi kushindwa kutoa ushirikiano kwa wamwagiliaji wakidai
kuwa dawa hizo zinasababisha ongezeko la wadudu kama kunguni katika nyumba zao
pamoja na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wananume.
Hayo yamebainishwa na
baadhi ya wanyunyuziaji wa dawa hizo mkoani hapa walipokuwa wakizungumza na Storm
habari mapema hii leo ambapo wamesema
kuwa wananchi wamekuwa wakishindwa kutoa
ushirikiano kutokana na kuamini kuwa dawa hizo zinasababisha upungufu wa nguvu
za kiume na ikiwemo kuongezea kwa wadudu hali ambayo inasabishwa zoezi hiloo
kushindwa kufanyika ipasavyo.
Hata hivyo storm habari
imezungumza na mratibu mthibiti wa malaria kutoka katika halimashauri ya mji wa
Geita bi Rachel Masuke ambapo amesema kuwa suala hilo halina ukweli wowote
ndani yake kwani dawa hizo zimetolewa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoeneza
magonjwa ikiwemo mbu pamoja na wadudu wengine.
Aidha Rachel amewataka
wananchi kuachana na imani hzo kwa kukubali nyumba zao zinyunyuziwe kwani lengo
la serikali ni kuhahaikisha inapunguza kasi ya maambukizi ya maralia nchini na
sio kuongeza wadudu.
No comments:
Post a Comment